Mkondo, Mohamed Muslim
(2025)
Athari za Mbinu za Kisanaa Katika Ujenzi wa Dhamira za Maigizo: Mifano Kutoka Igizo la Matusi la Madebe Lidai.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulimakinikia kuchunguza athari za mbinu za kisanaa zinazotumika katika ujenzi wa dhamira za maigizo. Mifano imetumika kutoka igizo la Matusi. Ili kufanikisha uchunguzi wa athari za mbinu hizo, utafiti huu ulijiegemeza katika kubainisha mbinu za kisanaa zilizotumika kujenga dhamira katika igizo la Matusi, kuchambua matumizi ya mbinu za kisanaa zilizojenga dhamira katika igizo la Matusi na kubainisha athari za matumizi ya mbinu za kisanaa katika ujenzi wa dhamira katika igizo la Matusi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya utazamaji na usikilizaji makini. Mkabala wa kimaelezo pamoja na nadharia ya simiotiki zilitumika katika kuchambua data za utafiti. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa mbinu za kisanaa ambazo zimetumika katika kujenga dhamira zimeegemezwa zaidi katika majazi, ujenzi wa wahusika kikorasi, takriri, nyimbo, tashibiha, tashihisi, tafsida, motifu, matumizi ya hadithi ndani ya hadithi na ngoma. Aidha, matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba mbinu za kisanaa zimekuwa na athiri chanya na hasi katika ujenzi wa dhamira katika igizo la Matusi. Athari chanya hizo ni kama vile kujenga moyo wa huruma kwa wanawake, kuimarisha ushawishi wa kisiasa, kujenga uelewa wa kihistoria, kudumisha ukarimu, ukombozi wa wanawake na kuongeza ushawishi na mvuto wa kimasimulizi. Na athari hasi ni kuwepo kwa dharau pamoja na mwanamke kuchorwa kama chombo cha starehe. Mwisho utafiti huu umependekeza kuwa ipo haja ya kufanywa utafiti wengine katika kuangalia mbinu za kisanaa katika maigizo megine ya Madebe Lidai. Pia, mtafiti anapendekeza kuwa tafiti linganishi zifanyike katika kuangazia matumizi ya mbinu za kisanaa katika igizo la Matusi na maigizo ya wasanii wengine ili kuiboresha fani ya fasihi ya Kiswahili.
Actions (login required)
 |
View Item |