Asajile, Subilaga Ramsy
(2025)
Kuchunguza Dhamira ya Maadili katika Nyimbo za Harusi za Jamii ya Wanyakyusa.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasinifu hii imechunguza dhamira ya maadili katika nyimbo za harusi za jamii ya Wanyakyusa. Ili kutimiza kusudi hilo kulikuwa na malengo mahususi mawili. Kwanza kubainisha nyimbo za harusi zilizomo katika jamii ya Wanyakyusa wa Wilaya ya Rungwe. Pili, kuchambua maadili yaliyomo kwenye nyimbo za harusi za jamii ya Wanyakyusa. Mkabala wa Kitaamuli umetumika katika utafiti huu. Data za msingi zilikusanywa kwa njia ya usikilizaji makini wa nyimbo teule. Uchambuzi, uhakiki na mjadala wa data zilizowasilishwa uliongozwa na nadharia ya Usosholojia. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuna nyimbo mbalimbali za harusi zinazopatikana katika jamii ya Wanyakyusa nyimbo hizo ni ubhumang'anyi, ubwikili, tumoghele, bhamanyene, kundangasya, ndeke abhukeghe, nakubhulile mwanangu, na Malaine. Pia utafiti huu umebaini kuwa nyimbo teule za harusi za Wanyakyusa zina utajiri mkubwa wa maadili yaliyoshikamana vyema na utamaduni, maisha na mazingira ya jamii iliyochunguzwa. Maadili hayo ni kama vile. Umuhimu wa uaminifu, upendo na ukarimu, matumizi sahihi ya simu, wosia kwa wanandoa, kuepuka usaliti na kuwa ushujaaa. Nyimbo za harusi za Wanyakyusa zinalenga kuifunza jamii masuala ya kijamii na kiutamaduni. Tasinifu hii inapendekeza kuundwa kwa mikakati thabiti inayolenga kuendeleza utamaduni wa taifa na sanaa zake pamoja na kulinda kazi za wasanii kisera na kisheria. Aidha wasanii wajenge utashi wa kuzitawala vyema kazi zao ili waweze kumudu ushindani wa kisanaa, kimaudhui na kiwakati.
Actions (login required)
 |
View Item |