Kuchunguza Ujumbe Unaojengwa na Muktadha katika Nyimbo za Asili za Sherehe za Wahehe.

Rashid, Mwajabu Majaliwa (2025) Kuchunguza Ujumbe Unaojengwa na Muktadha katika Nyimbo za Asili za Sherehe za Wahehe. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA MWAJABU MAJALIWA SAFI KABISA BLACK BOOK.docx] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (10MB)
Official URL: http://www.out.ac.tz

Abstract

Utafiti huu ulilenga “Kuchunguza ujumbe unaojengwa na muktadha katika nyimbo za asili za sherehe za Wahehe,” kwa kuongozwa na malengo mahususi mawili: kubainisha miktadha ya uwasilishaji wa nyimbo za asili za sherehe za Wahehe na kuelezea ujumbe unaopatikana katika nyimbo za asili za Sherehe za Wahehe. Mbinu za ukusanyaji wa data ulihusisha mbinu za ushiriki kwenye shughuli za sherehe za za Wahehe, ushuhudiaji na hojaji. Utafiti huu unajengwa na nadharia ya Mwitiko wa Msomaji. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba, nyimbo za asili za Sherehe za Wahehe hutumika katika Miktadha mbalimbali ya jamii hiyo kama vile: shughuli za ,matambiko,kilimo,misiba,jando na unyago,shghuli za ndoa ambapo mambo kadhaa hufanyika kama vile,kumuona binti, kuwatuma wazee kwenda nyumbani kwa wazazi wa binti kuzungumza nao, kuposa, kupangiwa mahari, kulipa mahari, kufanyiwa sherehe ya harusi, kwenda nyumbani na kuanza maisha ya ndoa. Aidha, nyimbo hizo zina ujumbe mzuri na muhimu kwa wanajamii wa asili ya Wahehe na Watanzania kwa ujumla, kwa kuwa Wahehe pia huoana na watu wengine wa maeneo ya nje na kabila lao. Utafiti umetoa mapendekezo zaidi kwa utafiti ujao katika eneo la fani katika nyimbo za harusi za jamii ya Wahehe hususani matumizi ya lugha kwani kuna utajiri mkubwa wa mbinu za matumizi ya lugha katika nyimbo hizo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Jan 2026 15:12
Last Modified: 30 Jan 2026 15:14
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/5008

Actions (login required)

View Item View Item