Kuchunguza Migogoro katika Riwaya za Kiswahili: Mifano Kutoka Katika Vuta N’kuvute.

Gabriel, Lucy (2025) Kuchunguza Migogoro katika Riwaya za Kiswahili: Mifano Kutoka Katika Vuta N’kuvute. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA LUCY GABRIEL FOR BLACK BOOK.docx] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (82kB)
Official URL: http://www.out.ac.tz

Abstract

Mada ya tasinifu hii ni kuchunguza migogoro katika riwaya ya Kiswahili kwa kurejelea riwaya ya Vuta N’kuvute ya mtunzi Shafi Adam Shafi. Malengo mahususi yalikuwa matatu ambayo ni kubainisha migogoro inayojitokeza katika riwaya teule, kufafanua vichocheo vya migogoro hiyo na kuelezea uhalisia wa migogoro hiyo kwa jamii ya leo. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Saikolojia Changanuzi. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa katika riwaya teule ya Vuta N’kuvute kunajitokeza migogoro nafsia, mtu na mtu, kifamilia na wakoloni na wananchi. Migogoro hii inaonekana kuwa na uhalisia hata katika maisha ya leo ya jamii ambapo wanajamii wanakumbana nayo kila uchao. Sasa hakuna wakoloni lakini wapo wanyonyaji ambao ni wawekezaji wenye sifa sawasawa na wakaloni na wanawanyonya sana wananchi. Kwa upande wa vichocheo vya migogoro katika riwaya teule, matokeo ya utafiti yamebainisha vichocheo hivyo kuwa ni mapenzi, ubaguzi, ukandamizaji, utamaduni na pombe. Vichocheo hivi ni halisia hata katika maisha ya leo ya jamii kwani migogoro mingi ambayo inatokea katika jamii huchochewa na kimoja kati ya vichocheo hivi. Mwishoni mwa tasinifu hii tumetoa hitimisho, muhtasari na mapendekezo kwa ajili ya utafiti wa baadae. Mapendekezo yaliyotolewa katika utafiti huu ni kwamba, utafiti kama huu ufanywe katika riwaya nyingine za Shafi Adam Shafi ili kuona namna migogoro inavyojengwa ndani ya riwaya zake. Sambamba na hilo, unaweza kufanywa utafiti ambao utaangalia athari za migogoro hiyo kwa jamii kama inavyowasilishwa katika riwaya husika. Pia, utafiti kama huu unaweza kufanywa katika riwaya za watunzi wengine wa riwaya za kisasa na kimapokeo kwa lengo la kulinganisha na kulinganua. Hii itatusaidia kuona ufanano na utofautiano wa ujengaji wa migogoro katika riwaya za kisasa na kimapokeo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Jan 2026 15:04
Last Modified: 30 Jan 2026 15:04
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/5007

Actions (login required)

View Item View Item