Mtazamo kuhusu matumizi ya Kiswahili Kufundishia na Kujifunzia Masomo ya Sekondari: Uchunguzi kutoka Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

Philemon, Joseph (2023) Mtazamo kuhusu matumizi ya Kiswahili Kufundishia na Kujifunzia Masomo ya Sekondari: Uchunguzi kutoka Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of JOSEPH PHILEMON.pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu ulikusudia kuchunguza Mtazamo kuhusu matumizi ya Kiswahili kufundishia na kujifunzia masomo ya sekondari. Walengwa wa utafiti huu walikuwa walimu, wanafunzi na wazazi katika shule za sekondari za serikali wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi matatu ambayo ni; Kubainisha sababu zinazoshawishi matumizi ya Kiswahili kufundishia na kujifunzia masomo ya sekondari, kubainisha vikwazo vinavyokwamisha lugha ya Kiswahili isitumike kufundishia na kujifunzia masomo ya sekondari na kutathmini mtazamo wa wanajamii kuhusu matumizi ya Kiswahili kufundishia na kujifunzia masomo ya sekondari. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya hatua iliyofikiriwa ambayo imeaksi vyema kusudio la utafiti huu. Njia ya dodoso, mahojiano na uchunzaji darasani zilitumika kukusanya data. Uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ulitumia mikabala ya kitakwimu na kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yalibaini sababu zinazoshawishi matumizi ya Kiswahili kufundishia na kujifunzia masomo ya sekondari ni; Kiswahili kuwa lugha bora, Kiswahili kutawala mazungumzo, Kiswahili kuwa lugha mama, Kiswahili kuwa na msamiati toshelevu, Kiswahili ni lugha muhimu na Kiswahili kueleweka kwa urahisi. Pili, utafiti ulibaini vikwazo vinavyokwamisha lugha ya Kiswahili isitumike kufundishia na kujifunzia masomo ya sekondari ni kulegalega kwa sheria ya lugha nchini Tanzania, udhaifu wa asasi na vyombo kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, Kiswahili kutokuwa na hadhi, kulegalega kwa sera ya lugha na msukumo mdogo wa viongozi wa kisiasa. Tatu, utafiti ulibaini upo mtazamo chanya wa wanajamii kuhusu matumizi ya Kiswahili kufundishia na kujifunzia masomo ya sekondari.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 21 Oct 2024 16:16
Last Modified: 21 Oct 2024 16:16
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4311

Actions (login required)

View Item View Item