Dhima za Nyimbo katika Matambiko ya Jamii ya Watu wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Mussa, Hidaya Juma (2023) Dhima za Nyimbo katika Matambiko ya Jamii ya Watu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of HIDAYA JUMA MUSSA.pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (565kB)

Abstract

Utafiti huu umechunguza dhima zaa nyimbo za matambiko katika jamii ya watu wa Mkoa Kusini Unguja. Lengo hilo lifikiwa kwa kubainisha nyimbo za matambiko zilizopo katika jamii ya watu wa Makunduchi. Sambamba na kubainisha mahali, wakati na jinsi nyimbo zinavyotumika katika Mkoa wa Kusini Unguja. Aidha, uchunguzi wa dhima zinazojitokeza katika nyimbo za matambiko katika jamii ya watu wa Mkoa wa Kusini zilifafanuliwa. Utafiti huu ulifanyika uwandani kwa kushuhudia, kuhoji na kudodosa ili kukusanya data kutoka vyanzo tofauti vya watafitiwa. Utafiti huu ulifanyika katika Kisiwa cha Unguja, Mkoa wa Kusini, Wilaya Kusini katika kijiji cha Makunduchi, Uchambuzi wa data za wa utafiti huu ni wa mkabala wa kimaelezo hii ni kutokana na aina ya utafiti pamoja na sampuli iliyotumika. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ya Simiotiki na ya Uhalisi mazingaombwe. Nadharia mbili hizi zimetumika ili kusaidia katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa tambiko ni amali muhimu katika ustawi wa maisha ya watu wa Kusini Unguja kwa sababu tambiko limetumika katika shughuli nyingi muhimu za kijamii. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa nyimbo za tambiko zipo za aina tofauti kama vile, za kukaribisha mizimu, maamkizi, dua, na kuomba shifa. Pia, eneo la utendekaji ni pwani, kwenye miti mikubwa, mapango na kwenye uwanja. Maneno Muhimu: Mizimu, Tambiko, Nyimbo

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 18 Oct 2024 10:21
Last Modified: 18 Oct 2024 10:21
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4286

Actions (login required)

View Item View Item