Kuchunguza Dhamira katika Hadithi za Watoto: Mfano kutoka Wilaya ya Temeke.

Warioba, Winifrida Mataso (2023) Kuchunguza Dhamira katika Hadithi za Watoto: Mfano kutoka Wilaya ya Temeke. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of WINIFRIDA MATASO WARIOBA.pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (990kB)

Abstract

Tasinifu hii ilihusu “Kuchunguza Dhamira katika Hadithi za Watoto: Mfano kutoka Wilaya ya Temeke.” Utafiti huu uliongozwa na lengo kuu na malengo mahsusi mawili, lengo kuu lilikuwa ni kuchunguza dhamira katika Hadithi za Watoto katika Wilaya ya Temeke na na malengo mahususi la kwanza ni Kuchambua dhamira katika hadithi za Watoto katika Wilaya ya Temeke na lengo la pili ni kubainisha ujumbe unaopatikana katika hadithi za Watoto katika Wilaya ya Temeke. Data za msingi za utafiti huu zilikusanywa kwa mbinu ya ushuhudiaji, dodoso na uchambuzi wa kinyaraka. Mjadala na uchambuzi wa data zilizowasilisha uliongozwa na nadharia ya Sosholojia ya Fasihi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa dhamira mbali mbali zilizoibuka kutokana na utafiti na uchambuzi uliofanywa. Dhamira hizo ni usafi wa mazingira, wizi katika jamii, ujasiriamali, mmonyoko wa maadili, ulevi katika jamii, uvivu na uzembe katika jamii na umoja na mshikamano. Ujumbe uliojitokeza katika hadithi za watoto ni pamoja na usafi wa mazingira ni jambo la muhimu katika jamii zetu ivo kila mtu ayapende mazingira yake, wizi ni tamaa na yaweza kumfikisha mtu pahala pabaya, majivuno siyo jambo zuri katika maisha, kiburi na dharau sio kitu kizuri katika maisha, umoja na mshikamano ni jambo la msingi mno Wananchi waishi kwa kushirikiana, ulevi ni adui wa maendeleo na ujumbe mwingine ni kila mtu anapaswa kujitegemea katika maisha na kufanya kazi kwa bidi. Utafiti huu umetoa mapendekezo kwa watafiti wengine na jamii kwa ujumla, wazidi kufanya tafiti zaidi kuhusu hadithi za watoto katika wilaya mbalimbali ili waweze kuzibainisha dhamira na mafunzo katika hadithi za Watoto, na kuvifanya vizazi vijavyo viweze kufaidika na hadithi hizo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 18 Oct 2024 10:11
Last Modified: 18 Oct 2024 10:11
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4285

Actions (login required)

View Item View Item