Kuchunguza Itikadi katika Mashairi ya Muhammed Seif Khatib: Mifano kutoka Diwani ya Wasakatonge.

Laizer, Meijo Loloinyo (2023) Kuchunguza Itikadi katika Mashairi ya Muhammed Seif Khatib: Mifano kutoka Diwani ya Wasakatonge. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of MEIJO LOLOINYO LAIZER.pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (771kB)

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza itikadi katika mashairi ya Muhammed Seif Khatib katika Diwani ya Wasakatonge. Katika kukamilisha tasnifu hii, utafiti ulikuwa na malengo mahususi mawili ambayo ni kuchambua masuala ya kiitikadi yanazojitokeza katika mashairi ya Wasakatonge na kubainisha mbinu za kisanaa zinazoibua masuala ya kiitikadi katika mashairi ya Wasakatonge. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka kwa kuongozwa na nadharia mbili za U-marx na Simiotiki. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba masuala yanayojenga itikadi katika mashairi ya Wasakatonge ni, uongozi mbaya, uchu wa madaraka na uongozi, mapenzi, matabaka, ukoloni mamboleo, malezi na maadili katika jamii. Pia matokeo ya utafiti huu, yanaonyesha kuwa itikadi katika mashairi ya Wasakatonge zinajengwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisanaa kama tamathali za usemi za tashibiha, sitiari, takriri na misemo tu ndizo zilizotafitiwa. Kupitia vipengele hivyo vya fani, mtunzi ameweza kuwasilisha itikadi mbalimbali katika kazi yake ya fasihi kwa Mashairi ya Wasakatonge.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 18 Oct 2024 10:03
Last Modified: 18 Oct 2024 10:03
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4284

Actions (login required)

View Item View Item