Ibrahim, Ulfat Abdulaziz
(2023)
Uchunguzi wa Migongano ya Kimbari katika Muktadha wa Zanzibar ya Ubaadaukoloni: Uchanganuzi wa Riwaya ya Vuta N’kuvute na Mungu Hakopeshwi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasinifu hii inahusu ‘Uchunguzi wa Migongano ya Kimbari katika Muktadha wa Zanzibar ya Ubaadaukoloni: Uchanganuzi wa Riwaya ya Vuta N’kuvute na Mungu Hakopeshwi’, Ili kutimiza kusudi hilo kulikuwa na malengo mahsusi matatu. Lengo la kwanza lilikuwa kubainisha makundi ya kimbari yanayoonekana katika jamii ya Zanzibar ya Baadaukoloni kupitia riwaya ya Vuta N’kuvute na Mungu Hakopeshwi, lengo la pili lilikuwa kuchanganua aina za migongano ya kimbari ya jamii ya Wazanzibari wa Baadaukoloni kupitia riwaya ya Vuta N’kuvute na Mungu Hakopeshwi na lengo la tatu lilikuwa kutathmini mikakati ya utangamano wa kimbari inayopendekezwa katika riwaya za Vuta N’kuvute na Mungu Hakopeshwi. Data za msingi zilikusanywa kwa mbinu ya usomaji makini na uchambuzi wa kinyaraka. Mjadala na uchambuzi wa data uliongozwa na nadharia ya Ubaadaukoloni. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba katika riwaya teule kuna makundi ya kimbari ya kundi la Waafrika au Waswahili, kundi la Waarabu, kundi la Wahindi na kundi la Machotara. Kwa upande wa aina za migogoro ya Kimbari tumebaini aina mbili ambazo ni hisia-kinzani katika utambulisho na hisia-kinzani katika ndoa na mapenzi. Matokeo ya utafiti yanaendelea kuonesha kwamba mikakati ya kuondoa migongano hiyo ni kufanya mabadiliko ya tabia na utambulisho mpya wa Wanajamii kuwa na mapenzi yasiyokuwa na mipaka ya kimbari na uvunjaji wa mila za kinasaba. Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi katika eneo hili la umbari na fasihi ufanyike zaidi na pia kutoa elimu kwa umma juu ya watu wote kuishi kwa pamoja na kushirikiana katika mambo ya kijamii kutasaidia katika kupunguza na hata kuondoa migongano ya kimbari.
Actions (login required)
|
View Item |