Vigezo vya Utoaji wa Majina ya Watu katika Jamii ya Wamatengo.

Mbunda, Elvis Regnard (2023) Vigezo vya Utoaji wa Majina ya Watu katika Jamii ya Wamatengo. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ELVIS EDITED TASNIFU FINAL2. (SUBMIT).pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (942kB)

Abstract

Utafiti huu ulichunguza vigezo vya utoaji wa majina ya watu katika jamii ya Wamatengo. Utafiti ulikuwa na malengo mahususi matatu; kubainisha vigezo vinavyotumika kutoa majina ya watu katika jamii ya Wamatengo,kufafanua maana za kiishara zinazofumbatwa na majina ya watu na kujadili umuhimu wa maana za majina ya watu katika jamii ya Wamatengo. Utafiti huu ulifanyika katika wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma katika maeneo ya Kihangimahuka, Linda, Lukasrasi na Mahande. Mbinu za usomaji makini, usaili na mahojiano ya vikundi zilitumika katika ukusanyaji wa data ambapo data hizo zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Nadharia ya Semiotikiilitumika katika uchambuzi na uwasilishaji wa data. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwavigezo vinavyotumika kutoa majina ya watu ni pamoja na tabia au sifa, hisia au imani za wazazi, mazingira na matukio yaliyojiri wakati mtoto anazaliwa. Vigezo vingine ni kazi aliyonayo mtu, maumbile au rangi ya mwili, kipindi mtoto alichozaliwa na mahali alipozaliwa mtoto huyo. Pamoja na vigezo hivyo, imani za dini za wazazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kiasi fulani yameanza kuviathiri vigezo Utafiti umebaini kuwa, majina ya watu yamefumbata maana za kiishara ambazo huakisi historia na maisha ya kila siku katika jamii ya Wamatengo. Pia, maana za majina ya watu zina umuhimu mkubwa katika jamii ya Wamatengo kwa sababuhutambulisha, kuendeleza na kuhifadhi utamaduni wa jamii Wamatengo, kuadibu na kuelimisha jamii.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 06 Sep 2024 10:21
Last Modified: 06 Sep 2024 10:21
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4182

Actions (login required)

View Item View Item