Changamoto katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Somo la Kiswahili katika Shule za Sekondari Tanzania: Uchunguzi Kifani Wilaya ya Temeke.

Ndomba, Neema Samuel (2023) Changamoto katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Somo la Kiswahili katika Shule za Sekondari Tanzania: Uchunguzi Kifani Wilaya ya Temeke. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of NEEMA SAMUEL NDOMBA tyr.pdf] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu ulichunguza changamoto katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari wilaya Temeke. Lengo la utafiti lilikuwa kutathmini changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari za Temeke na malengo mahususi yalikuwa ni kutathmini changamoto za upatikanaji wa nyenzo za kufundishia kwa walimu wa somo la Kiswahili, kuchunguza changamoto za upatikanaji na matumizi ya nyenzo za kujifunzia, kutathmini ubora wa maandalizi ya walimu kuhusu ufundishaji na kubainisha maoni ya watafitiwa kuhusu utatuzi wa changamoto walizoibua. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Utabia inayosisitiza upataji na mabadiliko ya uwezo wa tabia inayotokana na michakato ya ujifunzaji na mazoea yanayoimarishwa. Sampuli ya utafiti ilikuwa watafitiwa 120, (wanafunzi 100, walimu 15 na wakuu wa shule 5) kutoka shule tano katika kata ya Mibulani. Mbinu ya unasibu ilitumika kuwateua. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia njia ya usaili na mahojiano. Uchambuzi wa data umefanyika kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kitakwimu. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa suala la nyenzo za kufundishia bado ni tatizo. Pia upatikanaji na matumizi ya nyenzo za kujifunzia ni tatizo linalowakabili wanafunzi. Utafiti umebaini mafunzo kwa walimu ni suala ambalo halipewi kipaumbele katika kuimarisha ufundishaji. Ilibaini kuwa nyenzo za kufundishia na kujifunzia bado ni tatizo ambalo lina kwamisha ufundishaji na ujifunzaji. Utafiti unatoa mapendekezo kwa serikali na wakuu wa shule kuhakikisha upatikanaji na uenezaji wa nyenzo za kujifunzia na kufundishia. Walimu wa Kiswahili waongezewe mafunzo ya kuimarisha ujuzi wao kwa kupitia warsha au semina.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 06 Sep 2024 10:10
Last Modified: 06 Sep 2024 10:10
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/4180

Actions (login required)

View Item View Item