Kuchunguza Namna Uhalisia mazingaombwe Unavyoibua Maudhui katika Hadithi Simulizi za Jamii ya Wazanzibari

Faki, Bikombo (2023) Kuchunguza Namna Uhalisia mazingaombwe Unavyoibua Maudhui katika Hadithi Simulizi za Jamii ya Wazanzibari. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of BIKOMBO JUMA FAKI.docx] HTML - Submitted Version
Download (209kB)

Abstract

Tasnifu hii imejikita katika ‘Kuchunguza uhalisia mazingaombwe na namna unavyoibua maudhui katika hadithi simulizi zinazopatikana katika jamii za Wazanzibari’ Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu: Moja, ‘Kubainisha vipengele mbalimbali vya kifani vilivyoonesha uhalisiamzaingaombwe katika hadithi simulizi tulizoziteua. Mbili, Kuchambua vipengele vyauhalisia mazingaombwe vinavyoibua maudhui ndani ya hadithi simulizi teule. Tatu Kubainisha miktadha ambayo uhalisia mazingaombwe huelekezwa katika hadithi simulizi teule. Data za utafiti zilikusanywa kwa mbinu za hojaji na usaili. Pia mtafiti katika kazi hii ametumia njia ya uwandani na ile ya maktabani. Mjadala wa data ulioongozwa na nadharia ya Uhalisia mazingaombwe. Nadharia hiyo ilikuwa muafaka katika uchambuzi na mjadala wa vipengele vilivyolengwa katika utafiti huu. Nadharia hiyo iliteuliwa kwa misingi ya kutegemeana na kukamilishana ili kukidhi malengo mahsusi ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa vipengele vya kifani vimetumika kuonesha uhalisia mazingaombwe katika hadithi simulizi za jamii ya Kizanzaibari. Pia uhalisia mazingaombwe umeibua maudhui ya mapenzi ya kweli, umoja na mshikamano, ugumu wa maisha, kupigania haki na ujasiri na ukakamavu. Utafiti huu unapendekeza kuwa watafiti wengine wazidi kufanya tafiti zaidi juu yauhalisia mazingaombwe katika hadithi simulizi za jamii ya Wazanzibari kupitia vipengele vyake, kwa mfano, wahusika wa uhalisia mazingaombwe nao wahusishwe na wanajamii wa uswahilini, pia tafiti nyengine zifanyike kuhusu mabadiliko ya uhalisia mazingaombwe kwa kuyahusisha na sayansi na teknolojia. Maneno Muhimu: Teknolojia, mazingaombwe, fani

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 410 Linguistics
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Khadija Katele
Date Deposited: 31 Jul 2024 11:51
Last Modified: 31 Jul 2024 11:51
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3900

Actions (login required)

View Item View Item