Massoud, Sauda Rashid
(2022)
Kuchunguza Taswira katika Nyimbo za Taarab za Kimahaba za Khadija Kopa.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasnifu hii inahusu Kuchunguza Taswira katika Nyimbo za Taarab za Kimahaba za Khadija Kopa. Utafiti ulilenga kuzibainisha taswira zinazotumiwa na Khadija Kopa katika nyimbo za mahaba za Khadija Kopa, kubainisha miktadha ya matumizi ya taswira katika nyimbo za taarab za mahaba za Khadija Kopa. Na kuchunguza athari za taswira hizo kwa jamii. Mbinu iliyotumika kupata data ni usomaji makini. Mtafiti alizisikiliza huku akizinukuu nyimbo za taarab 21 za Khadija Kopa katika mtandao wa “You Tube” na kuchagua nyimbo 5 ambazo ndizo alizoziwasilisha na kuzifanyia uchambuzi kwa njia ya maelezo na majadwali. Nyimbo hizo ni Niliwaze, Nimemridhi, Mwanamke Mambo, I Love You na Full Stop. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya Simiotiki. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa nyimbo za mahaba za Khadija Kopa zinatumia taswira za za kizuolojia, taswira za botania, taswira za kiastromia, taswira za kijiolojia, taswira ya kiteolojia na taswira za vitu vya kawaida. Pia, matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa miktadha inayosababisha ubunifu wa taswira katika nyimbo za Khadija Kopa ni miktadha ya mapenzi, miktadha ya utamaduni, miktadha ya utandawazi, miktadha ya imani na miktadha ya kifasihi. Kwa upande wa athari za taswira hizo kwa jamii, utafiti umebaini kuwa kuna athari chanya na hasi. Athari chanya ni pamoja na kukuza lugha, kuendeleza utamaduni, kukuza fasihi, kutambulisha na kuifunza jamii. Kwa upande wa athari hasi ni kuhamasisha ngono holela, kuendeleza mawazo ya kumfanya mwanamke kuwa chombo cha starehe dhidi ya mwanamme, kutumia lugha ya matusi na kuchochea migogoro. Mwisho utafiti umependekeza kuwa ipo nafasi ya kufanya tafiti nyengine katika nyimbo za taarab zikiwa na malengo tofauti na utafiti huu kama vile kuchunguza majigambo ya watrib wa nyimbo za taarab hasa za wanawake akiwemo Khadija Kopa.
Maneno Makuu: Taarab, Majigambo, Nyimbo
Actions (login required)
|
View Item |