Makosa ya Kifonolojia Yanayofanywa na Wazungumzaji wa Kihaya Wanaojifunza Kiswahili Sanifu

Felician, Frederick (2019) Makosa ya Kifonolojia Yanayofanywa na Wazungumzaji wa Kihaya Wanaojifunza Kiswahili Sanifu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of fredrick.pdf] PDF
Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu umechunguza wa makosa ya kifonolojia yanayofanywa na wazungumzaji wa Kihaya wanaojifunza Kiswahili sanifu. Malengo ya Utafiti huu yalikuwa ni (a) Kubainisha makosa ya kifonolojia yanayofanywa na wazungumzaji wa Kihaya katika ujifunzaji wa Kiswahili sanifu (b) Kubainisha sababu za wazungumzaji wa Kihaya kufanya makosa ya kifonolojia katika kujifunza Kiswahili sanifu (c) Kubainisha mbinu za kutumia ili kuwasaidia wazungumzaji wa Kihaya wanaojifunza Kiswahili sanifu kama L2 kwao. Njia zilizotumika kukusanya data ni hojaji ilitumika kwa watafitiwa ambao ni wanafunzi, walimu na wazazi, mahojiano ambayo ilitumika kwa walimu na wazazi wazungumzaji wa Kihaya na Kiswahili na usomaji makini ambayo ilitumika kupitia kwa umakini kazi mbalimbali za wanafunzi ili kubaini makosa ya kifonolojia. Data ya utafiti huu imechanganuliwa kwa makabala wa kimaelezo kwa kuongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makosa ya Corder (1967). Matokeo ya utafiti yanaonesha makosa yanayofanywa kuwa ni pamoja na matumizi ya sauti mbadala kwa sauti ambazo hazipo katika mfumo wa lugha ya Kihaya ila zipo katika Kiswahili sanifu, kuchanganya sauti, udondoshaji na uchopekaji wa sauti. Sababu za wazungumzaji wa Kihaya kufanya makosa ya kifonolojia katika kujifunza Kiswahili sanifu zipo kama ifuatavyo; utofauti wa mifumo ya sauti kati ya lugha hizi mbili, ufundishaji mbaya wa lugha ya pili, walimu kutokuwa na taaluma ya fonetiki matamshi na matumizi ya Kihaya muda mwingi kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla. Mbinu za kuwasaidia wanafunzi hawa ni pamoja na wazazi, wanafunzi na jamii nzima ya wazungumzaji wa lugha ya Kihaya kutambua umuhimu wa Kiswahili, taaluma ya fonetiki matamshi kutolewa ngazi zote za elimu, matumizi ya mbinu bora za ufundishaji wa lugha ya pili.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 23 Sep 2021 09:31
Last Modified: 23 Sep 2021 09:31
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3014

Actions (login required)

View Item View Item