Mangi, Joyce Elia
(2019)
Athari za Lugha ya Kinyaturu katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya
Pili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu uulilenga kuchunguza athari ya lugha ya Kinyaturu katika ujifunzaji wa
lugha ya Kiswahili ili kubainisha changamoto na mwisho kutoa mapendekezo ya
suluhisho la changamoto hizo. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu;
Kwanza, kubainisha athari za lugha ya Kinyaturu katika ujifunzaji wa lugha ya
Kiswahili kwa wanafunzi wanaozungumza Kinyaturu kama lugha yao ya kwanza.
Pili, kubainisha sababu za athari hizo kwa wazungumzaji wa Kinyaturu wanaojifunza
lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili. Tatu, kupendekeza mbinu mbalimbali
zitakazotumika kuwasaidia wanafunzi walioathiriwa na Kinyaturu wanapojifunza
lugha ya Kiswahili. Aidha, utafiti huu ulifanyika katika eneo la Singida Vijijini
ambapo data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu kuu tatu; usomaji wa
maandiko, mahojiano na hojaji. Wahojiwa waliteuliwa kwa njia ya usampulishaji
makusudi na nasibu. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano
(NKM). Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, athari za lugha ya kinyaturu
katika ujifunzaji wa kiswahili ziko kwenye kisemantiki (kimaana), kimsamiati, na
kimatamshi. Mtafiti aliweza kubaini mbinu ambazo zinaweza kutumika katika
kuwasidia wanafunzi walioathilika kwa lugha ya awali wanapojifunza lugha ya
kiswahili. Mbinu hizo ni, watoto wafundishwe lugha ya Kiswahili tangia utotoni,
walimu wanapaswa kuwa mahiri katika kufundisha lugha ya kiswahili, kuwe na
mazingira rafiki ya kujifunza lugha ya kiswahili, wazazi au walezi wa watoto
wahamasishwe kutumia lugha ya kiswahili. Kwa mujibu wa utafiti huu zipo sababu
zinazosababisha kutokea kwa athari za lugha ya kinyaturu katika kujifunza lugha ya
kiswahili kama ufundishaji mbaya wa somo la kiswahili, lugha ya kiswahili
kutopewa kipaumbele, kudumisha utamaduni wa kinyaturu, mazingira duni ya
kujifunza lugha ya kiswahili, lugha ya kinyaturu hutumika kama utambulisho
Actions (login required)
|
View Item |