Salim, Asha Khamis
(2018)
Mfumo Angami wa Kipemba na Athari zake katika Kuzuia Mawasiliano Fanisi kwa Wageni wa Lahaja hio.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unaohusu “Muachano wa Kiisimu unaojitokeza kati ya Kiswahili Sanifu na Kipemba‟, lengo lake kuu ni kuchunguza “Muachano wa Kiisimu unaojitokeza kati ya Kiswahili Sanifu na Kipemba. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya mbili. Nadharia ya kwanza ni ile ya Isimulinganishi na nadharia ya Mofofonolojia. Utafiti umetumia mbinu za mahojiano, hojaji na ushuhudiaji katika ukusanyaji wa data zake. Utafiti umefanyika Madenjani, Mchangamdogo Kiuzu, Mjiniole na Kangagani. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, data zimeonesha kuwa kuna kuna muwachano wa kifonolojia kwenye mpishano wa baadhi ya sauti kwenye neno hilo hilo moja. Kuna mpishano wa kimofolojia kwenye viambishi njeo na nafsi, kuna muachano kwenye matumizi ya vivumishi, vitenzi vishirikishi zaidi kwenye matumizi ya viangama. Kwa upande wa mapendekezo mtafiti amependekeza ufanyike utafiti wa muachano baina ya Kiswahili na lahaja mbalimbali za visiwani kama vile Kimakunduchi na lahaja nyengine za Kiswahili.
Actions (login required)
|
View Item |