Kuchunguza Uhalisiajabu katika Riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale

Said, Rahma Mohammed (2019) Kuchunguza Uhalisiajabu katika Riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA RAHMA MOHAMED SAID.pdf] PDF
Download (437kB)

Abstract

Utafiti huu unahusu kuchunguza uhalisiajabu katika Riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale. Utafiti huu ulihusisha malengo mahsusi mawili ambayo ni kubainisha vipengele vya uhalisiajabu katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale na lengo la pili ni kubainisha dhamira zinazojidhihirisha kutokana na matumizi ya vipengele vya Uhalisiajabu katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale. Katika kuyabainisha na kuyachambua malengo haya, mtafiti ametumia mbinu ya usomaji makini pamoja na upitiaji wa nyaraka maktabani. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalumu. Aidha, data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu uliongozwa na Nadhariaya Uhalisiajabu kwa lengo mahsusi la kwanza na suali la kwanza. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji imetumika kwa lengo mahsusi la pili na suali la pili katika muktadha wa Uchambuzi wa Matini za Kifasihi. Utafiti umegundua kuwariwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale imetumia vipengele vya uhalisiajabu ambavyo ni wahusika wa kihalisiajabu, mandhari ya uhalisiajabu, uzungumzi nafsi, matukio ya kihalisiajabu, usimulizi wa kihalisiajabu na umahuluti wa kitanzu, kitamaduni na mwingilianomatini. Adha, utafiti umegundua kuwa vipengele hivyo vya uhalisiajabu katika riwaya teule vimeibua dhamira za imani za jadi, uongozi mbaya, ukoloni, utabaka, mauaji, umuhimu wa kutunza kumbukumbu, upelelezi, uganga wa kienyeji, unyonyaji na ukandamizaji na nafasi ya mwanamke. Kwa matokeo haya utafiti huu umebaini kwamba riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale imesawiriwa kwa mbinu ya uhalisiajabu kwa kiasi kikubwa kama mtindo wa msanii kuibua dhamira alizozikusudia kwa jamii aliyoiandikia.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 11:25
Last Modified: 21 Sep 2021 11:25
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2912

Actions (login required)

View Item View Item