Upimaji wa Uelewa wa Matumizi ya Mofu Nafsi na Njeo za Kiswahili kwa Wanafunzi wa Zanzibar

Adi, Aziza Masoud (2018) Upimaji wa Uelewa wa Matumizi ya Mofu Nafsi na Njeo za Kiswahili kwa Wanafunzi wa Zanzibar. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA AZIZA MASOUD ADI.pdf] PDF
Download (809kB)

Abstract

Tasnifu hii ni matokeo ya utafiti uliolenga kuchunguza “upimaji wa uelewa wa matumizi ya mofu nafsi na njeo za Kiswahili kwa wanafunzi wa :mifano kutoka Zanzibar”. Utafiti uliofanywa uliongozwa na malengo makuu mawili ambayo ni; Kuainisha kiwango cha uelewa wa maumbo ya mofu nafsi na njeo katika Kiswahili Sanifu kwa wanafunzi wa Zanzibar, na Kubainisha changamoto za ujifunzaji na ufundishaji wa mofu nafsi na njeo za Kiswahili Sanifu katika shule za Zanzibar.Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni pamoja na usaili kwa walimu na hojaji kwa wanafunzi, pia mtafiti alitumia mbinu ya maktabani katika maandiko mbalimbali ili kupata data za upili.Mbinu hizi zilichangia mtafiti kujua kiwango cha uelewa wa wanafunzi katika matumizi ya maumbo ya mofu nafsi na njeo katika Kiswahili Sanifu pamoja na changamoto zake. Nadharia zilizotumika katika uchambuzi wa data za utafiti huu ni nadharia ya mofofonolojia na nadharia ya Linganuzi. Sampuli iliyotumika katika utafiti huu, ni ya walimu 24 (30%) na wanafunzi 56 (70%), ambao kwa ujumla ni sawa na watafitiwa 80 (100%). Matokeoya utafiti yanaonesha kwamba wanafunzi wanauwelewa wa 56.25% katika uchambuzi mofu nafsi na wastani wa 52.08% kwenyeuchambuzi wa mofu njeo. Utafiti ulibaini kuwa changamoto kubwa inayowakabili walimu na wanafunzi ni suala la uhaba wa vitabu rejea kwa walimu na hata wanafunzi wakati wa kujifunza mada hii. Kutokana na matokeo haya, utafiti huu unashauri mambo yafuatayo; kwanzawanafunzi kushirikishwa katika vitendo zaidi kuliko kufundishwa au kujifunza kwa nadharia.Pia Taasisi husika iengeze vitabu rejea vyakutosha vinavyohusiana na mada ya mofu. Halikadhalika wadau wa elimu wawe na uhusiano wa kutosha na walimu katika kuhamasisha ujifunzaji wa mada ya mofu kwa kutoa vipeperushi pamoja na kuandaa na kuwasilisha warsha na makongamano yanavyoonesha uchambuzi na uchanganuzi wa maumbo ya mofu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 11:01
Last Modified: 21 Sep 2021 11:01
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2909

Actions (login required)

View Item View Item