Maana za kimuktadha zilizojitokeza katika semi zilizoandikwa katika majina ya kanga

Haji, Amina Makame (2019) Maana za kimuktadha zilizojitokeza katika semi zilizoandikwa katika majina ya kanga. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA AMINA MAKAME HAJI.pdf] PDF
Download (288kB)

Abstract

Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza Maana za Kimuktadha zilizojitokeza katika Semi zilizoandikwa katika Majina ya Kanga. Utafiti huu ulikuwa na malengo matatu ya msingi. Malengo hayo ni Kubainisha semi mbali mbali zilizoandikwa katika kanga kutegemeana na maudhui zake. Kubainisha maana za semi teule zilizoandikwa kwenye kanga kwa kuangalia maana ya msamiati na muktadha na Kuchambua maana za muktadha ya semi teule zilizoandikwa kwenye kanga. Mbinu za kukusanyia data za utafiti huu zilkuwa ni mahojiano na uchunguzi makini. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa mkabala wa kimaelezo huku ukiongozwa na nadharia tatu. Nadharia hizo ni Maana Kimatumizi, Maana Kimuktadha na nadharia ya Simiotiki. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa kuna semi mbalimbali zilizotofautiana kimaudhui ambazo zimeandikwa katika kanga. Semi hizo zimejikita katika maudhui ya mila na utamaduni wa jamii, dini na imani, maarifa mengineyo, bidii katika kazi na subirá na uvumilivu. Kwenye lengo la pili, matokeo yalionesha kuwa maana za semi zinajikita kimsamiati na kimuktdha. Maana za kimsamiati huibuka kutokana na vijenzi mahususi vilivyojenga usemi wenyewe. Maana za kimuktadha zinatokana na tafsiri mahususi inayotokana na mtazamo na muktadha wa kimatumizi kama inavyofahamika na jamii husika. Na katika lengo la tatu amegundua kuwa semi zilizo katika maudhui mbalimbali huandikwa kwenye kanga ili kufikisha ujumbe maalum kwenye jamii ambapo kanga huvaliwa. Semi hizo kukanya, hukosoa na hata kuelekeza juu ya utendaji bora wa mambo katika jamii husika. Kwa mfano maswali ya wivu uliokomaa ulizungumziwa, umuhimu wa kubaki kwenye ndoa, umuhimu wa kuheshimiana, umuhimu wa bidii ya kazi, subirá na uvumilivu na maadili kadha ya kijamii yalihusishwa kwenye lengo hili la tatu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 08:18
Last Modified: 21 Sep 2021 08:32
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2895

Actions (login required)

View Item View Item