Athari ya Kiswahili Sanifu Katika Msamiati wa Lahaja Ya Kimakunduchi

Chum, Zubeida Moh’d (2019) Athari ya Kiswahili Sanifu Katika Msamiati wa Lahaja Ya Kimakunduchi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ZUBEIDA MOH’D CHUM-TASINIFU.pdf] PDF
Download (676kB)

Abstract

Utafiti huu ulichunguza Athari ya Kiswahili Sanifu katika Msamiati wa Lahaja ya Kimakunduchi. Utafiti ulikuwa na lengo la kutathmini athari za Kiswahili sanifu katika msamiati wa lahaja ya Kimakunduchi. Ili kukamilisha lengo hilo, utafiti uliongozwa na malengo mahsusi matatu, ambayo ni; Kubainisha njia zilizotumika kuathiri msamiati wa lahaja ya Kimakunduchi kutokana na maingiliano ya Kiswahili sanifu, kubainisha msamiati ulioachwa na ulioibuka kutokana na maingiliano ya Kiswahili sanifu katika lahaja ya Kimakunduchi. Na, kutathmini athari za Kiswahili sanifu katika msamiati wa lahaja ya Kimakunduchi. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Mwathiriano wa lugha. Nadharia hii ilitosheleza katika ukusanyaji wa data na uchambuzi wake. Pamoja na nadharia hii, utafiti ulitumia mbinu zilizowezesha kukusanya data na kuzichambua. Mbinu hizo ni, hojaji, mahojiano, mjadala wa vikundi na ushuhudiaji. Mbinu na nadharia hii, zilimuezesha mtafiti kujua namna ya upatikanaji wa data, kuzikusanya na kuzichambua hadi kukamilika kwa kazi nzima. Matokeo ya utafiti yalipatikana kutokana na data zilizokusanywa kutoka maktabani na uwandani. Matokeo hasa ya uwandani yalitoa jibu la tatizo lililokuwa likishughulikiwa kwa usahihi zaidi. Hii ni kwa sababu mtafiti alifika katika sehemu husika ambako Kimakunduchi kinazungumzwa. Matokeo ya utafiti yaligundua kuwa, kuna baadhi ya msamiati wa kale ambao kwa sasa umeachwa au hutumika kwa nadra kutokana na muingiliano wa Kiswahili sanifu katika lahaja hii. Vilevile, kuna msamiati ambao umeibuka katika lahaja ya Kimakunduchi, msamiati huu haukuwa ukitumika katika lahaja ya Kimakunduchi hapo kabla. Sababu kuu ya kuibuka ni muingiliano wa Kiswahili sanifu kutokana na njia mbali mbali ikiwemo shughuli za kiuchumi, utamaduni na masuali ya kijamii. Kutokana na matokeo hayo, mtafiti aligundua kuwa kuna athari nyingi za muingiliano huu ikiwemo; kupotea kwa msamiati wa asili wa lahaja ya Kimakunduchi na kupoteza vyanzo vya msamiati kwa lugha ya Kiswahili sanifu. Hali hii itaifanya lahaja ya Kimakunduchi kuwa hatarini kupotea au kufa kabisa. Mwisho, utafiti umetoa mapendekezo ambayo yataisaidia lahaja ya Kimakunduchi kubaki hai, kujiimarisha na kukiimarisha Kiswahili kwa kukitunzia vyanzo vyake vya kuingiza msamiati, kutunza utamaduni na kuchangia utanuzi wa mawanda ya lugha na matumizi yake.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 09 Dec 2020 13:14
Last Modified: 09 Dec 2020 13:14
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2604

Actions (login required)

View Item View Item