Athari ya Kubadili Msimbo katika Mawasiliano

Kassim,, Shaaban Juma (2017) Athari ya Kubadili Msimbo katika Mawasiliano. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Shabani Juma Kassim.docx] PDF - Submitted Version
Download (165kB)

Abstract

Kubadili msimbo ni kati ya mtindo wa lugha uliozoeleka sana katika jamii ya watu wenye uwili lughaingawaje jamii nyingi sasa zimeingia katika eneo la matumizi ya lugha kwa sababu mbali mbali. Kutokana na hali hiyo mfumo wa matumizi ya lugha umekua ukichukua sura tofauti kila uchao kutokana na maendeleo sayansi na teknolojia. Pia ongezeko la maingiliano ya watu kutoka sehemu mbali mbali za ulimwenguni na haja ya mawasiliano. Kwa sababu ya kupanuka kwa wigo huo matumizi ya lugha hufanywa katika mitindo tofauti jambo ambalo limezaa changamoto na athari katika Isimujamii, mawasiliano na katika Kiswahili kwa ujumla. Mabadiliko ya sarufi na mgawanyiko wa makundi ya watu ni moja ya changamoto na athari hizo. Ili kujua athari za matumizi hayo ya lugha, utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza matumizi ya kuchanganya au kubadili msimbo na athari zake katika Kiswahili. Utafiti umeongozwa na nadharia kadhaa. Nadharia hizo ni pamoja na nadharia sarufi amilishi mfumo (SAM), Nadharia Kidhi ya Mawasiliano (NKM), na ubadilikaji zenye lengo la kueleza sababu za kubadili na au kuchanganya msimbo wakati wa mawasiliano na kuangalia athari zake katika jamii. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa kusini Pemba, katika wilaya ya Mkoani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, mahojiano na uchunguzi. Matokeo yameonesha kuwa matumizi ya kuchanganya msimbo yana athari kwa jamii na lugha ya Kiswahili ujumla. Kutokana na matokeo hayo, inapendekezwa kuwa vianzishwe vitengo maalumu vitakavyoshughulikia mitindo mbalimbali inayoibuka katika lugha ili kuihifadhi na kuidhibiti mitindo lugha.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 04 Mar 2020 13:34
Last Modified: 04 Mar 2020 13:34
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2476

Actions (login required)

View Item View Item