Kuchunguza Mabadiliko ya Kasida Visiwani Zanzibar Baada ya Mapinduzi na Wakati wa Soko Huria

Hamad,, Othman Suleiman (2017) Kuchunguza Mabadiliko ya Kasida Visiwani Zanzibar Baada ya Mapinduzi na Wakati wa Soko Huria. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of OTHMAN SULEIMAN HAMAD.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (511kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu una lengo la Kuchunguza Mabadiliko ya Kasida kwa kuchunguza fani na dhamira. Utafiti huu una malengo manne ambayo ni kubainisha kasida mbalimbali zilizosomwa katika kipindi cha baada ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kipindi kilichoshughulikiwa ni kuanzia miaka ya 1970 na wakati wa soko huria na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuanzia miaka ya 1990-2016, kuainisha vipengele vya fani vilivyotumika katika awamu hizo mbili, kubainisha dhamira za kasida katika awamu hizi mbili na kubainisha mabadiliko ya kifani na kidhamira kasida katika kipindi cha awamu mbili. Ili kufikia lengo kuu lililokusudiwa, mbinu za utafiti zilizohusika ni hojaji, usaili na kushiriki katika matukio ya usomwaji wa kasida. Nadharia mbili zilizoongoza utafiti huu ni nadharia ya umuundo na nadharia ya sosholojia ya fasihi na sampuli iliyotumika ni watu mia moja, kati ya hao hamsini wanawake na hamsini wanaume. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, mtafiti aligundua kwamba kuna mabadiliko katika kasida. Mabadiliko hayo yanajitokeza katika fani na dhamira zake. Matumizi ya vifaa vya kisasa vya muziki kama vile kibodi, vinanda, nai na vipaza sauti vimebadilisha mtazamo wa kasida baada ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Soko huria limezifanya kasida ziwe ni biashara kuliko kushughulika na dini. Mtafiti amependekeza mambo kadhaa kwa watafiti wajao na jamii wayatupie macho na kuyafanyia kazi. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuwaomba watafiti na wahakiki kujadili na kutilia mkazo uandishi wa tanzu hizi za kasida kama vinavyofafanuliwa vipengele vyengine. Walimu na wanafunzi wa mad-rasa wazingatie malengo ya kasida ili zibaki katika uhalisia wake, pia jamii zijali, kuheshimu na kuzingatia mipaka ya usomaji wa kasida

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 04 Mar 2020 12:23
Last Modified: 04 Mar 2020 12:23
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2462

Actions (login required)

View Item View Item