Kuchunguza Taswira ya Mwanamke na Mbinu za Kifani katika Mashairi: Mfano wa Diwani ya Midulu

Kimaro, Florian August (2016) Kuchunguza Taswira ya Mwanamke na Mbinu za Kifani katika Mashairi: Mfano wa Diwani ya Midulu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU MPYA YA KIMARO-20-12-2016-2.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (451kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulizungukia lengo kuu ambalo lililenga kuchunguza taswira ya mwanamke katika Diwani ya Midulu. Lengo kuu la utafiti huu lilikwenda sambamba na malengo mahususi matatu ambayo yalikuwa ni kubainisha taswira ya mwanamke katika mashairi ya Tigiti Sengo kama inavyosawiriwa katika Diwani ya Midulu, kuelezea sababu zilizofanya taswira ya mwanamke iwe hiyo inayosawiriwa katika diwani hiyo na kuchambua mbinu za kifani zilizotumiwa na mwandishi katika kujenga taswira ya mwanamke katika Diwani ya Midulu. Malengo mahususi ya utafiti huu yameshughulikiwa ipasavyo baada ya kukusanya data za utafiti kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Data zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Ufeministi. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa mwanamke amesawiriwa kama kiumbe mlezi, mwanamke na stara, mwanamke na kazi, uzuri wa mwanamke ni tabia na subira, mwanamke na uongozi na mwanamke na upendo. Sababu za mwanamke kusawiriwa hivyo ni kutokana na mafundisho ya dini, hali ya utandawazi, mabadiliko ya jamii kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Sababu hizi zimelezwa moja kwa moja katika uchambuzi wa data za lengo mahususi la kwanza kutokana na ukaribu wake kimaana. Vipengele vya mbinu za fani vilivyochambuliwa katika utafiti huu ni muundo wa takhmisa, tarbia na tathilitha, wahusika katika Diwani ya Midulu, mtindo; matumizi ya lugha ya kawaida, kiitikio na kibwagizo na matumizi ya lugha ya mafumbo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 09 Oct 2018 07:09
Last Modified: 09 Oct 2018 07:09
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2201

Actions (login required)

View Item View Item