Kuchunguza Maudhui ya Nyimbo za Kampeni za Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2000-2010

Ali, Daud Moh’d (2017) Kuchunguza Maudhui ya Nyimbo za Kampeni za Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2000-2010. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU -  Daud Mohammed Ali.pdf]
Preview
PDF
Download (1MB) | Preview

Abstract

Utafiti huu umechunguza maudhui ya nyimbo za kampeni za uchaguzi mkuu, Zanzibar (2000-2010). Mtafiti aliongozwa na madhumuni mahsusi matatu, la kwanza, kuchunguza na kuainisha nyimbo za kampeni za uchaguzi mkuu, Zanzibar 2000-2010, la pili, Kutathmini mchango wa nyimbo za kampeni za uchaguzi mkuu Zanzibar, katika kustawisha jamii ya Wazanzibari, na la tatu, Kutafuta mbinu za kufanya nyimbo hizo ziwe zinaleta umoja badala ya utengano katika jamii ya Wazanzibari. Katika kufanikisha madhumuni hayo, mtafiti alifuata njia zilizostahiki kwenda kwenye vikundi vya ngoma na kukutana na malenga ili kupata data alizozihitaji kwa watafitiwa. Watafitiwa hao waligawanyika katika makundi ya vijana, watu wazima wenye maarifa na kumbukumbu za mambo ya kihistoria, walimu, wasanii, wataalamu wa lugha ya Kiswahili na utamaduni, na waandishi wa habari. Mtafiti aliongozwa na nadharia ya mtu na Utamaduni, nadharia ya Fasihi ina kwao, nadharia ya Tabia na nadharia ya Uhalisia katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti. Aidha, utafiti umetaja kipengele cha lugha, wahusika na mandhari ili kuibulia maudhui yaliyokusudiwa. Utafiti umeonesha dhamira ya kuhamasisha, ajira kwa vijana, na mmomonyoko mkubwa wa maadili ya jamii. Mwisho, utafiti umetoa mapendekezo kwa watafiti wa usoni.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 17:23
Last Modified: 05 Oct 2018 17:23
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2122

Actions (login required)

View Item View Item