Kuchunguza Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Alikiona

Massuod, Ismahan Abulkasim Essa (2018) Kuchunguza Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Alikiona. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ISMAHAN ABULKASIM ISSA MASSED.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (480kB) | Preview

Abstract

Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona. Katika kufanikisha lengo hili, utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi mawili ambapo lengo la kwanza lilikuwa ni kuchambua usawiri wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona na kuelezea uhalisia wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona kwa jamii ya leo. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji matini na upitiaji wa nyaraka. Data za utafiti zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Ufeministi. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usawiri wa mwanamke unajitokeza katika maeneo ya mwanamke ni uzinzi, mwanamke ni mtu wa hila na ghilba, mwanamke ni mpenda ufahari, mwanamke ni muongo, mwanamke na mmbeya, mwanamke na ujanja, mwanamke ni mtunza kumbukumbu, mwanamke ni stara, mwanamke ni mpenda kupigwa na mwanamke ni mtoa matusi. Usawiri huu wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Alikiona umethibitika kuwa na uhalisia katika maisha halisi ya jamii ya Watanzania ambapo mwanamke halisi anafanana na mwanamke ambaye anatajwa katika tamthiliya. Wapo wanawake kadhaa ambao wamekuwa na sifa kama hizo za mwanamke anayetajwa katika Alikiona.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 04 Oct 2018 16:51
Last Modified: 04 Oct 2018 16:51
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2070

Actions (login required)

View Item View Item