Kuchunguza Dhamira na Fani katika Nyimbo za Taarab Asilia: Mifano ya Nyimbo za Shakila Saidi Khamisi

Abdalla, Asha Rashid (2018) Kuchunguza Dhamira na Fani katika Nyimbo za Taarab Asilia: Mifano ya Nyimbo za Shakila Saidi Khamisi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ASHA RASHID ABDALLA-TASNIFU-13-02-2018.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (983kB) | Preview

Abstract

Lengo la utafiti huu ni Kuchunguza Dhamira na Fani katika Nyimbo za Taarab asilia za Shakila Saidi Khamisi. Ili kukamilisha lengo hili, utafiti huu ulikuwa na malengo mahsusi mawili ambayo ni (i) Kuchambua dhamira katika nyimbo teule za Shakila Saidi Khamisi na (ii) Kubainisha mbinu za kisanaa zinazojitokeza katika nyimbo teule za Shakila Saidi Khamisi. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka maktabani. Utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo. Hoja zilijengwa na kujengewa misingi imara ya kinadharia. Nadharia iliyotumika katika uchambuzi wa data ni zile za Mwitiko wa Msomaji na Simiotiki. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa kuna dhamira mbalimbali zinazojitokeza katika nyimbo za taarab asilia za Shakila Saidi, miongoni mwa dhamira hizo ni pamoja na zile zinazohusiana na mapenzi, utamaduni, usaliti, dini na imani, elimu, ukweli na uwazi, ukombozi, umalaya na dhamira nyenginezo. Pia utafiti huu umebaini mbinu za kisanaa zilizomo katika nyimbo za taarab asilia za Shakila Saidi. Miongoni mwa mbinu hizo za kisanaa ni tamathali za semi kama vile kejeli, tashtiti, majazi, taswira na ishara, sala, takriri na nyenginezo. Vile vile utafiti umegundua kuwa msanii Shakila Saidi alibobea sana katika matumizi ya mbinu za kisanaa na kanuni za kimapokeo jambo ambalo lilirahisisha ujengaji wa dhamira za nyimbo zake.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 01 Oct 2018 15:05
Last Modified: 01 Oct 2018 15:05
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2020

Actions (login required)

View Item View Item