kutathmini nafasi ya mwanamke na matumizi ya lugha katika tamthiliya za Kwenye Ukingo wa Thim na Wangari Maathai: Utafiti Linganishi

Isaac, Sinna Mgambi (2017) kutathmini nafasi ya mwanamke na matumizi ya lugha katika tamthiliya za Kwenye Ukingo wa Thim na Wangari Maathai: Utafiti Linganishi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Tasnifu ya Sinna-30-10-2017 (1).doc] PDF - Submitted Version
Download (376kB)

Abstract

Utafiti huu unachunguza nafasi ya mwanamke na matumizi ya lugha katika tamthiliya za Kwenye Ukingo wa Thim na Wangari Maathai: Utafiti linganishi. Utafiti huu ambao ni utafiti linganishi uliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni:Mosi;Kubainisha nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa jamii katika tamthiliya mbili teule.Pili,Kulinganisha na kulinganua nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa jamii katika tamthiliya mbili teule.Tatu,Kulinganisha matumizi ya lugha za kisanaa katika tamthiliya mbili teule na lengo kuu ni kutathmini nafasi ya mwanamke na matumizi ya lugha katika tamthiliya za Kwenye Ukingo wa Thim na Wangari Maathai.Katika kutekeleza malengo hayo tuliteua sampuli ya utafiti kwa mbinu ya kusudio. Sampuli hiyo ndiyo iliyotumiwa kukusanyia data za msingi, data hizi zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji wa matini na kuchambuliwa kwa mkabala wa kimaelezo na midafao. Uhakiki wa data katika Utafiti huu uliongozwa na nadhariya mbili ambazo ni nadhariya ya Ufeministi ambayo imetumika kubainisha nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa jamii katika tamthiliya teule. Nadhariya ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha na kulinganua nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa jamii katika tamthiliya teule pamoja na matumizi ya lugha ya kisanaa yaliyojitokeza katika tamthiliya teule tilizozitumia. Matokeo ya uatafiti huu yameonyesha kwamba, mosi, waandishi wa tamthiliya teule tukianza na mwandishi Emmanuel Mbogo yeye anamsawiri mwanamke kama mtu mwenye jukumu kubwa la kutetea haki za binadamu, demokrasia na haki za binadmu, kusimama kidete katika jukumu la kuandaa taifa la kesho. Na kwa upande wa mwandishi Ebrahim Hussein yeye anaainisha majukumu ya mwanamke katika mtazamo ufuatao: mwanamke anajukumu la kuitetea nchi yake, kuchapa kazi, kusimamia maadili na kuleta mabadiliko katika jamii yake. Pili, Utafiti huu umebaini kuwa utofauti wa nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa jamii umejitokeza kupitia jukumu la utetezi wa haki za binadamu, demokrasia, utunzaji wa mazingira na uongozi,majukumu haya yamejitokeza katika tamthiliya ya Wangari Maathai pekee. Na kwa upande wa tamthiliya ya Kwenye Ukingo wa Thim, jukumu pekee la mwanamke ambalo limejitokeza katika tamthiliya hii ni jukumu la kusimamia maadili ya jamii. Kwa upande wa ufanano, ufanano wa majukumu ya mwanamke katika ujenzi wa jamii umejitokeza kupitia majukumu kadha wa kadha miongoni mwa majukumu hayo ni: uzalendo, uchapa kazi na chachu ya mabadiliko katika jamii inayowazunguka. Tatu, Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa, waandishi wa tamthiliya teule kwa pamoja wametumia matumizi ya lugha ya dhihaka, jazanda, takriri na misemo katika kufikisha ujumbe walioukusudia kwa jamii zao na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuufikisha ujumbe muafaka kwa jamii walioiandikia.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Sep 2018 08:16
Last Modified: 30 Sep 2018 08:16
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2003

Actions (login required)

View Item View Item