Tathmini ya Mabadiliko ya Maana ya Msamiatiwa Kiswahili Katika Muktadha wa Kisiasa: Mifano Kutoka Katika Hotuba za Kampeni Uchaguzi 2015

Rajab, Wema Twaha (2017) Tathmini ya Mabadiliko ya Maana ya Msamiatiwa Kiswahili Katika Muktadha wa Kisiasa: Mifano Kutoka Katika Hotuba za Kampeni Uchaguzi 2015. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIF - WEMA RAJAB - final.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (920kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulitathmini mabadiliko ya maana ya msamiati katika muktadha wa kisiasa.Malengo ya utafiti yalikuwa ni kutathmini mwelekeo wa mabadiliko ya maana mpya ya msamiati katika muktadha wa kisiasa na lengo la pili ni kuchunguza ukubalikaji wa maana mpya ya msamiati baada ya uchaguzi kwisha. Utafiti huu umeongozwa na nadharia tatu, nadharia ya Foucault (1981) ya mwenendo na mabadiliko, nadharia ya Dorwn (1838) ya ubadilikaji, pia nadharia kidhi ya mawasiliano ya (NKM) ya Giles ya mwaka (1973).Jumla ya hotuba sita zilisikilizwa na kuibua msamiati 84 iliobadilika maana katika muktadha wa kisiasa.Aidha, watafitiwa 85 walishirikishwa katika utafiti huu. Data zilikusanywakwa kutumia mbinu ya usikilizaji na usaili na pia mbinu ya maktabani. Pia data ziliainishwa kwa njia ya kitakwimu na njia isiyo ya kiidadi (maelezo) ikihusisha malengo yaliyowekwa na utafiti. Utafiti umegundua kuwa mabadiliko ya maana ya msamiati ambao umekusanywa katika hotuba umesababisha mabadiliko ya kisemantiki.Miongoni mwa mabadiliko hayo kuimarika kwa maana, udhalilikaji wa maana na usogezi wa maana. Aidha utafiti umegundua pia kati ya watafitiwa70 sawa na asilimia 82.35% wamesema kuwa msamiati uliobadilika maana katika maana muktadha wa kisiasa unakubalika katika jamii.Mtafiti anapendekeza kuwa watafiti wengine kuchunguza vipengele vya mofolojia na fonolojia katika muktadha huu. Pia kuchunguza mabadiliko ya maana mpya ya msamiati katika muktadha wa ofisini, sokoni na kwingineko.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Sep 2018 08:09
Last Modified: 30 Sep 2018 08:09
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2001

Actions (login required)

View Item View Item