Uchanganuzi wa Kirai cha Kibantu – Mtazamo wa X-baa Mfano: Kutoka Kirai Nomino na Kirai Kitenzi cha Kinyakyusa

Kanichi, Mary Nathaniel (2018) Uchanganuzi wa Kirai cha Kibantu – Mtazamo wa X-baa Mfano: Kutoka Kirai Nomino na Kirai Kitenzi cha Kinyakyusa. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Mary Kanichi-TASNIFU-24-01-2018.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (1MB) | Preview

Abstract

Uchanganuzi wa Kirai Nomino na Kirai Kitenzi cha Kinyakyusa ni mada ambayo iliyofanyika kwa kushirikisha watafitiwa 10 wazawa wa lugha hiyo wakiwemo walimu na wanafunzi wenye ufahamu wa dhana ya virai. Wazee watano (5), vijana watatu (3) na watoto wawili (2) kutoka katika kijiji cha Ipinda, kata ya Ipinda wilaya Kyela, mkoa wa Mbeya walishirikishwa. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza na kuchanganua virai vya kibantu mfano kutoka katika kirai nomino (KN) na kirai kitenzi (KT) cha Kinyakyusa kwa kutumia nadharia ya X-baa. Virai hivi vya Kinyakyusa vimeweza kubainishwa na kuonyesha vinavyojitokeza katika lugha hiyo. Pia virai hivyo vimeainishwa kwa kuzingatia miundo yake na kuchanganuliwa kwa kutumia nadharia ya X-baa. Imeonekana kuwa nadharia ya hii ya X-baa inautoshelevu wa kuweza kuchanganua, kufafanua na kuelezea virai vya lugha nyingi za kibantu, mfano kutoka katika virai hivi vya Kinyakyusa. Nadharia hii inaelezea kuhusu uwili kuwa kifundo hugawika katika matawi mawili pekee hivi ni kusema kuwa KN hakiwezi kuzalisha matawi matatu. Maelezo haya yametumika katika kuchanganua virai hivi vya Kinyakyusa. Virai vimeweza kubainishwa kwa kuonyeshwa vinavyojitokeza katika lugha hiyo, kuainishwa kwa kuzingatia miundo yake na pia kuchanganuliwa kikamilifu kwa kutumia nadharia hii ya X-baa. Matokeo ya utafiti huu yamegusia tu uchanganuzi wa virai viwili yaani kirai nomino (KN) na kirai kitenzi (KT) cha Kinyakyusa. Hivyo utafiti ufanyike zaidi katika uchanganuzi wa virai vingine na tungo ambazo utafiti huu haukushughulikia katika lugha hii ya Kinyakyusa kwa kutumia nadharia ya X-baa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 29 Sep 2018 11:10
Last Modified: 29 Sep 2018 11:10
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1971

Actions (login required)

View Item View Item