Kuchunguza Ujinsia na Matumizi ya Lugha katika Methali za Wakurya

Felician, Timanywa (2017) Kuchunguza Ujinsia na Matumizi ya Lugha katika Methali za Wakurya. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TIMANYWA_FELICIAN_RWEGIRA-Tasnifu-23-01-2017.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (663kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu kuchunguza ujinsia katika methali za Wakurya ambapo lengo kuu lilikuwa ni kuchunguza jinsi ujinsia katika methali za Kikurya unavyijitokeza katika mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume. Katika harakati za kukamilisha lengo hili data za utafiti zilikusanywa kwa mbinu ya hojaji pamoja na maswali ya madodoso kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini. Utafiti huu umetumia nadharia mbili yaani nadharia ya Ufeministi na nadharia ya Simiotiki. Matokeo ya utafiti yaanaonyesha kuwa ujinsia katika methali za Kikurya unajitokeza katika mahusiano kutokana na wanawake kunyanyasika, kuaonewa, kusalitiwa na hata kudharaulika kupitia vitu dhaifu na vinyonge. Kulingana na uchambuzi wa data, matokeo yanaonyesha kuwa ujinsia katika mahusiano baina ya mwanamke na mwanaume unatokana na vipaumbele vya jamii kuegemezwa katika upande mmoja yaani kwa wanaume na kuruhusu mwanamke kuamriwa baadhi ya mambo na mwanaume. Mila na desturi pia zimeonekana kuwa chachu ya uwepo wa ujinsia kupitia methali na mahusiano ya kijamii. Mwanamke anaonekana sana kuwa muathirika japo mwanamme anaonekana kuwa msababishi mkubwa wa viashiria vya ujinsia. Jamii inaonekana kumchukulia mwanamke kama mtu asiye na kwao kwa kuamini kuwa pindi anapoolewa na kutolewa mahari ndio unakuwa mwanzo wake wa kupata makazi ya kudumu. Ujinsia pia unajitokeza kupitia mbinu anuwai za kisanaa ambazo husawiri wanaume kupitia vitu vyenye nguvu, uwezo na ujasiri mwingi ilhali wanawake wakionekana kusawiriwa kwa vitu vidhaifu, vinyonge vinyonge, laini na vyenye mvuto. Tamathali za semi zilizotafitiwa ni pamoja na sitiari, kejeli, tashbiha, tafsida na balagha au chuku. Mtafiti amebainisha jinsi ujinsia unavyojitokeza kupitia tamathali hizo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Mar 2017 07:41
Last Modified: 23 May 2017 08:57
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1842

Actions (login required)

View Item View Item