Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Singo Katika Kijiji cha Uzini Zanzibar

Waziri, Mwaka Mwinyi (2016) Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Singo Katika Kijiji cha Uzini Zanzibar. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of UTAFITI_-_MWAKA_-FINAL.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (943kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulifanywa kwa lengo la kuchunguza dhima za nyimbo za singo katika kijiji cha Uzini Zanzibar. Katika kutimiza lengo hilo data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usaili, hojaji pamoja na mbinu ya ushuhudiaji katika maeneo ya Uzini Mshomarini, Mitakawani, Tunduni, Mpapa na Mgeni Haji, ambapo sherehe za singo zilifanyika. Data zilizokusanywa zilichambuliwa kwa kutumia mbinu za mkabala wa kimaelezo. Nadharia za Fasihi Ina Kwao, Dhima na Kazi pamoja na nadharia ya Uhalisia wa Kiafrika zilitumika katika kubainisha dhima hizo kwa jamii ya watu wa Uzini, ambazo zilisaidia kubaini utamaduni wa Mswahili kupitia kijiji hicho. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba nyimbo za singo ambazo ni sehemu ya fasihi simulizi, zina siri kubwa na ni mwalimu tosha wa kumpatia mwanamwari taaluma ifaayo kukabiliana na maisha yake ya ndoa. Kwa vile utafiti huu ulichunguza dhima za nyimbo za singo ukimlenga hasa mtoto mwanamke, utafiti umetoa hitimishi la moja kwa moja kwamba, jamii ya Waswahili hasa ya Kizanzibari, bado inaendeleza utamaduni wa kuwasinga wanawari kwa kutumia nyimbo ambazo zinatoa mafundisho yaliyo mema kwa lengo la kuwaandaa na maisha yao katika ndoa. Vilevile, utafiti umependekeza tafiti zaidi zifanyike kwa vijana wa jinsia ya kiume na kuangalia mafanikio kwa wanandoa waliofanyiwa mila na dasturi hii. Utafiti huu una manufaa kwa jamii hususani kwa vijana ambao wanajiandaa kukabiliana na maisha mapya ya ndoa, kwa vile uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa, nyimbo za singo zilitoa mchango mkubwa wa mafunzo kwao. Zinalenga kuwaandaa katika kuyakabili maisha yao kiuhalisia zaidi. Katika kufanikisha utafiti huu mtafiti alikabiliwa na matatizo kama vile ya uhaba wa wataalamu wa fani hiyo ya nyimbo za singo, maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo yaliaathiri sana upatikanaji wa taarifa za utafiti huu kwa vile wazee ambao ni mahiri kwa kutongoa nyimbo hizo walionekana kupoteza nafasi zao kwa kuwa na ushiriki mdogo katika shughuli hizo na kupelekea kupotea kwa nyimbo hizo katika vichwa vyao na kusababisha upotevu wa nyimbo za asili za singo. Aidhani, utafiti huu ulikabiliwa na tatizo la uhaba wa marejeleo yanayokwenda sawia na mada ya utafiti huu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Mar 2017 07:43
Last Modified: 23 May 2017 08:52
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1838

Actions (login required)

View Item View Item