Kuchunguza fani na dhamira katika semi zilizoandikwa katika vyombo vya safari vya Baharini Kisiwani Pemba

Juma, Nassor Hamad (2016) Kuchunguza fani na dhamira katika semi zilizoandikwa katika vyombo vya safari vya Baharini Kisiwani Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of UTAFITI_WA_NASSOOR_PEMBA_3_GLORY_-_Copy.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (508kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unalenga kuchunguza fani na dhamira katika semi za vyombo vya safari vya baharini kisiwani pemba semi hizo zinatumika katika shughuli za maisha ya wapemba ambapo zimeibua dhamira mbalimbali. Utafiti huu ulikua na malengo kama yafuatayo:lengo kuu la utafiti huu ni kuchukunguza fani na dhamira katika semi za vyombo vya safari vya baharini kisiwani pemba. Malengo mahasusi ni: 1. kubainisha semi katika vyombo vya safari vya baharini kisiwani Pemba 2. Kuonesha mbinu za kisanaa zilizotumika katika semi za vyombo vya safari vya baharini kisiwani Pemba 3. Kueleza dhamira zinazopatikana katika semi za vyombo vya safari vya baharini kisiwani Pemba.Utafiti huu umefanyika Tumbe wilaya ya Micheweni na Kojani wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Mbinu zilizotumika katika kukusanya data ni mbinu ya uwandani na mbinu ya maktabani, njia zilizotumika ni mahojiano na uchunguzi makini. utafiti huu ulitumia sampuli ya wazee vijana na walimu wa somo la kiswahili shule za sekondari.Nadharia zilizotumika katika utafiti huu ni nadharia ya simiotiki na nadharia ya muitiko wa msomaji. Kwa ujumla matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa Wapemba wanazo semi zinazotumika katika vyombo vya baharini. Semi zilizoandikwa katika vyombo vya baharini, zimetumika mbinu mbalimbali za kisanaa, mbinu hizo ni pamoja na tashtiti,taswira, kejeli, methali, misemo,simo, sitiri na kadhalika. Pia mtafiti aligundua kuwa semi hizo zina dhamira mbalimbali.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Mar 2017 07:43
Last Modified: 23 May 2017 08:50
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1836

Actions (login required)

View Item View Item