Athari za Itikadi katika Nyimbo za Harusi za Kizanzibari

Abdulla, Layla Msabah (2016) Athari za Itikadi katika Nyimbo za Harusi za Kizanzibari. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINFU_-_laila_binding.docx] PDF - Submitted Version
Download (175kB)

Abstract

Utafiti huu unahusu Athari za Itikadi katika nyimbo za Harusi za Kizanzibari. Utafiti ulifanyika katika visiwa vya Unguja na Pemba. Kwa upande wa kisiwa cha Unguja, utafiti ulifanyika katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Magharibi katika shehia za Mwanyanya na Mfenesini. Kwa upande wa kisiwa cha Pemba, utafiti ulifanyika katika Mkoa wa Kusini, Wilaya ya Chake Chake katika shehia ya Tibirinzi. Utafiti ulitumia mbinu ya usaili na ushiriki ambapo watoa taarifa 40, wanawake wenye umri kati ya miaka 20 – 60 walitumika katika kutoa data zilizokamilisha utafiti huu. Katika ukusanyaji na uchambuzi wa data, njia iliyotumika ni njia ya maelezo, kwani ndiyo muafaka kwa utafiti huu. Utafiti umegundua kuwa, nyimbo za harusi za Kizanzibari, huimbwa katika miktadha tafauti, kama vile, wakati wa kuwekwa ndani mwari harusi, kwa ajili ya mafunzo na matayarisho ya harusi, wakati wa kwenda kuowa, wakati wa kurudi na bibi harusi, tukitaja kwa uchache. Aidha, utafiti umegundua kuwa, nyimbo za harusi za Kizanzibari zimebeba itikadi nyingi, kama vile, itikadi juu ya umuhimu wa utii, umuhimu wa kuwa msafi, umuhimu wa kuheshimu ndowa, umuhimu wa mashirikiano, na itikadi juu ya umuhimu wa kuwa na uvumilivu katika ndowa, tukitaja kwa uchache tu.Aidha, utafiti huu umegundua kuwa matumizi ya lugha katika nyimbo za harusi za Kizanzibari, ni muhimu katika kuzifanya nyimbo zifahamike kwa wanandoa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Feb 2017 12:34
Last Modified: 23 May 2017 12:08
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1610

Actions (login required)

View Item View Item