Tofauti za Sentensi za Lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu Zinavyokwamisha Mawasiliano Fanisi baina ya wazungumzaji wa Kiswahili

Khalfan, Saida Said (2015) Tofauti za Sentensi za Lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu Zinavyokwamisha Mawasiliano Fanisi baina ya wazungumzaji wa Kiswahili. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of Tasnifu_2_of_2_1__-_desktop.pdf]
Preview
PDF
Download (541kB) | Preview

Abstract

Utafiti ulihusu uchunguzi juu ya ‘Tofauti za Sentensi za Lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu Zinavyokwamisha Mawasiliano Fanisi [Baina ya wazungumzaji wa Kiswahili]’. Sentensi ni kipashio cha juu cha kimuundo chenye maana kamili. Sentensi ni kipashio cha juu cha uzungumzaji katika lugha yoyote iwayo. Wazungumzaji wanaongozwa na kanuni za lugha wanayoitumia. Kanuzi hizo huzizingatia katika kuteua maneno, kupanga mofu ili kuunda maneno, kupanga maneno ili kuunda virai, kupanga virai ili kuunda vishazi na mwisho kupanga vishazi ili kuunda sentensi. Wazungumzaji wa lugha moja wanaweza kufanana katika kufuata taratibu za lugha lakini wakatofautiana katika uteuzi na mpangilio wa vipashio vya lugha yao. Jambo hili linapelekea kuwa na tofauti baina ya wazungumzaji wa lahaja ya Kipemba na wazungumzaji wa Kiswahili sanifu. Hali hii inapojitokeza bila shaka mawasiliano fanisi yanaweza kukosekana. Data nyingi zilizotumika katika utafiti huu zilikusanywa uwandani. Maeneo tofauti ya kisiwa cha Pemba yalihusishwa. Mbinu tuliyoitumia katika ukusanyaji wa data ilikuwa ni hojaji. Ugawaji wa dodoso uliwahusisha watu wachache sana. Ushuhudiaji pamoja na uzoefu wetu kwa maeneo ya utafiti pamoja na lahaja ya Kipemba na Kiswahili sanifu viliturahisishia zoezi la ukusanyaji data na udhibiti wake. Mbinu ya durusu ya maandiko ilitusaidia wakati wa kusoma kazi za waandishi mbalimbali. Data zilikusanywa kwa mwongozo wa nadharia ya makutano na mwachano, na kuchambuliwa kwa mbinu ya maelezo kwa mwongozo a nadharia ya sarufi muundo virai.Uchunguzi wetu ulibaini kuwa pamoja na kuwa Kiswahili sanifu na lahaja ya Kipemba ni mitindo ya lugha ya Kiswahili; pamoja na kuwa lahaja ya usanifishaji (Kiswahili sanifu) ni lahaja iliyokuwa ikizungumzwa Unguja Mjini (Kiunguja [cha wakati huo]) ambapo maeneo ya lahaja mbili hizi (lahaja ya Kipemba na lahaja ya Kiunguja [cha wakati huo]) yanakaribiana sana na watu wake wanachanganyika sana kutokana na sababu za kibiashara, kisiasa na kijamii; bado ipo tofauti kubwa baina ya miundo ya sentensi za Kiswahili sanifu na miundo ya sentensi za lahaja ya Kipemba. Tunaamini kuwa hitimisho la utafiti huu linakidhi mahitaji ya kitaaluma kutokana na hoja zilizojengwa juu ya dhana tuliyoichunguza.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:02
Last Modified: 13 Jul 2016 10:02
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1478

Actions (login required)

View Item View Item