kaguo, Joyce
(2015)
Mchango wa Mashairi ya Bi Madina Ali El-Buhriy Katika Arudhi ya Kiswahili Tanga.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza dhamira zinazojitokeza katika mashairi ya Bi Madina Ali El-Buhriy na namna tamatali za usemi zinavyosaidia kujenga dhamira hizo. Tumefikia malengo kwa kuibua dhamira kumi na mbili na kuchambua tamathali za usemi nane. Tasinifu hii ina sura kuu sita. Katika Sura ya Kwanza kuna utangulizi wa jumla, historia fupi ya Bi Madina Ali El-Buhriy, Usuli wa mada ya
utafiti, Usuli wa tatizo la utafiti, Tatizo la utafiti, Nia kuu ya utafiti, Malengo maalumu ya utafiti, Maswali ya utafiti, Umuhimu wa utafiti, Eneo la utafiti. Sura ya
Pili, kuna Uhakiki wa kazi za mashairi, Utafiti uliofanyika katika ushairi na hitimishi. Kuna mikabala ya kinadharia, Maana ya Nadharia, Ufafanuzi wa Nadharia. Sura ya Tatu, kuna maelezo juu ya mbinu na njia zilizotumiwa na mtafiti katika ukusanyaji wa data na zana za utafiti, Ratiba ya mtafiti, bajeti. Katika Sura ya Nne,kuna uwasilishaji wa matokeo ya utafiti, dhamira kumi na mbili zimejadiliwa;
Dhamira ya kutenda na kutendewa mema, Dhamira ya utunzaji wa Mazingira,Dhamira ya Kuhamasisha wanawake katika utunzi wa mashairi,Dhamira ya umalaya katika jamii, Dhamira ya umuhimu wa Wazazi, Dhamira ya hulka za binadamu,
Dhamira ya kumbukizi, Dhamira ya matatizo ya maji katika Jiji la Dar Es Salaam,
Dhamira ya Rushwa, Dhamira ya mabomu ya Mbagala, Dhamira ya
ugomvi/mafarakano. Katika Sura ya Tano, kuna matumizi ya fani, kipengele
kilichopewa uzito ni; lugha, tamathali za usemi zimechambuliwa kulingana na
muktadha wa utunzi wa mshairi, tashibiha, taswira, stiari, nidaa, takriri, tashihisi,
ritifaa, kejeli. Sura ya sita kuna maoni na mapendekezo kwa ajili ya jamii na tafiti
zijazo.
Actions (login required)
|
View Item |