Ali, Siti Faki
(2015)
Tofauti za Msamiati Wa lahaja ya Kipemba cha Kaskazini na Kipemba cha Kusini.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza tofauti za msamiati baina ya Kipemba cha Kaskazini na Kusini ikiwa ni hatua mojawapo ya kuitafiti lugha ya Kiswahili na lahaja zake ambapo kazi hii inatoa mawazo ya awali katika kuelezea tofauti za msamiati wa Kipemba kinachozungumzwa katika maeneo hayo. Data ya uwandani ya utafiti huu umekusanywa kwa kutumia mbinu za dodoso, mahojiano na ushuhudiaji ambapo sampuli-tegemea fursa na sampuli eneo zimetumika kuchagua watoa taarifa kwa vigezo vya umri, elimu na ukazi. Nadharia ya isimulinganishi, orodha ya Swadesh na mbinu za uchambuzi matini zimetumika kuchambua data hiyo. Katika kipengele cha msamiati ambacho kimechunguzwa, Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa kuna tofauti za msamiati baina ya Kipemba cha Kaskazini na Kusini. Hivyo, Kipemba cha Kaskazini kinaonekana kuhifadhi msamiati Kipemba cha kale (lahaja) ambapo Kipemba cha Kusini kinataka kufanana na Kitumbatu lakini kwa kiasi kikubwa kinaelekea kwenye usanifu. Kwa vile, utafiti huu unabainisha kuwa kuna tofauti za msamiati baina ya Kipemba cha Kaskazini na Kusini, utafiti huu hauhitaji hitimisho la haraka. Uchunguzi zaidi unahitajika kuchunguza asili ya watu na chimbuko la lahaja katika maeneo hayo.
Actions (login required)
|
View Item |