Itikadi katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo

Shemweta, Gladys (2015) Itikadi katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_GLADYS_SHEMWETA.pdf]
Preview
PDF
Download (783kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu Itikadi katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza itikadi katika tamthiliya mbili za Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo. Ili kukamilisha lengo hili data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji wa machapisho na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Utafiti huu umetumia nadharia mbili yaani nadharia ya Umarx na nadharia ya semiotiki. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa itikadi kama vile, ushirikina wa kichawi na kiganga, mapinduzi, ujamaa, ubepari, utamaduni, mapenzi na ndoa na dini zimejitokeza katika tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi. Kwa upande wa Fumo Liongo, itikadi za masuala ya sihiri, utawala wa milele, mapenzi ya dhati kwa jamii na malezi na uzazi zimejitokeza. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa itikadi ya uganga wa kichawi inafanana sana katika tamthiliya zote mbili ikilinganishwa na itikadi nyingine. Itikadi hii imetawala katika tamthiliya hizi, jambo linaloashiria kuwa hata katika jamii itikadi hii imetawala katika maisha ya watu waliowengi. Itikadi juu ya kuamini katika dini imejitokeza katika tamthiliya zote mbili kuthibitisha kuwa kwa asili mwanadamu ni mtu ambaye anazaliwa akiwa na itikadi juu ya uwepo wa Mungu. Pia, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa itikadi katika tamthiliya teuliwa zinajengwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisanaa. Katika utafiti huu tamathali za usemi za tashibiha, sitiari, kejeli, takriri na misemo tu ndizo zilizotafitiwa. Kupitia tamathali hizo, mwandishi ameweza kuwasilisha itikadi mbalimbali katika tamthiliya teuliwa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:34
Last Modified: 13 Jul 2016 10:34
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1289

Actions (login required)

View Item View Item