Mohd, Asha Rashid
(2015)
Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Ngoma ya Msondo wa Pembe.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu kuchunguza dhima za nyimbo za ngoma ya msondo. Utafiti ulifanyika katika shehia ya Kengeja, Mwambe na Mkungu- Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini- Pemba. Lengo kuu la utafiti huu ni kukusanya, kuchunguza na kuzianisha dhima za nyimbo za ngoma ya msondo [wa kike]. Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni nadharia ya Uamilifu, nadharia ya Simiotiki (Uashiriji), na nadharia ya Sosholojia (Ujamii). Data zilikusanywa kutoka uwandani kwa kutumia mbinu ya usaili na mbinu ya kushirki. Aidha njia ya maktabani ilitumika kwa kusomwa tasnifu
tafauti, vitabu na majarida. Matokeo ya utafiti ni dhima zilizopatikana ni dhima ya
kuelimisha kwa kuonya, kufunza, na kuhimiza maadili mazuri katika maisha ya
ndoa. Aidha, dhima ya kuburudisha maharusi imejitokeza katika nyimbo za ngoma
ya msondo. Mafunzo ya nyimbo hizi ambayo yamejitokeza ni ustahamilivu wa shida
na matatizo katika ndoa, kumuenzi na kumdhibiti mume au mke, kuwapenda na
kuwathamini wakwe, kutunza usafi na kujipamba mke mbele ya mume wake,
kuwacha tabia mbaya, kumuheshimu na kumtii mume. Kwa upande wa vipengele
vya fani vilivyosaidia kufikisha mafunzo kwa walengwa ni lugha ya ishara, taswira,
tashhisi, tauria, tashbiha, kejeli, na kadhalika kama vinavyojitokeza katika
uchambuzi wa vipengele hivyo katika sura ya nne.
Actions (login required)
|
View Item |