Kutathmini Usawiri wa Muhusika Mwanamke Katika Hadithi Simulizi za Wapemba

Ali, Hafsa Abdalla (2015) Kutathmini Usawiri wa Muhusika Mwanamke Katika Hadithi Simulizi za Wapemba. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_HAFSA_ABDALLA_FINAL.doc] PDF
Download (434kB)

Abstract

Utafiti huu ulihusu kutathmini usawiri wa muhusika mwanamke katika hadithi simulizi za Wapemba. Mtafiti alichagua mada hii ili kuchambua usawir huo kupitia hadithi simulizi. Utafiti huu una lengo kuu moja na madhumuni mahsusi matatu. Pia mtafi alitumia nadharia tatu katika utafiti wake. Nadharia ya Ufeministi wa Kiislamu, nadharia ya kijamii (ukhalisia) na nadharia ya mwitiko wa msomaji. Mtafiti alitumia njia kuu mbili katika utafiti wake, njia ya maktabani na njia ya maskanini. Katika njia hizo mtafiti alitumia mbinu mbalimbali kuzipata data zake. Mbinu hizo ni pamoja na hojaji na ushiriki darasani kwa upande wa njia ya maskanini na usomaji vitabu na tasnifu (kazi tangulizi) kwa njia ya maktabani. Data zilifanyiwa uchambuzi kwa njia ya maelezo na tarakimu, majadweli yalitumika kuonesha data hizo. Pia mtafiti ameweza kuonesha watafitiwa wake alivyowapata na jumla ya watafitiwa hao walikuwa arubaini na tano.Uchambuzi wa data ulifanyika kulingana na madhumuni mahsusi yaliyotajwa katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa muhusika mwanamke ameweza kusawiriwa kwenye nafasi kadhaa, miongoni mwa nafasi hizo, mwanamke ni mlezi, chombo cha starehe, jasiri, mwenye huruma, kiumbe duni, mchawi, katili, mchoyo, mfitinishaji, pambo, msaliti, mroho, mwanaharakati, mshiriki katika maamuzi na mshawishi.Aidha mtafiti ametumia hadithi simulizi za Wapemba, kuonesha usawiri huo na pia ametumia matukio halisi kutoka katika jamii ya Wapemba, kuonesha uhalisia wa nafasi hizo. Pia ameweza kugundua mbinu ya majazi kuwa ndiyo mbinu iliyotumika sana kusawiri wahusika katika hadithi simulizi za Wapemba.Mwisho amehitimisha kazi yake kwa kuweza kutoa mapendekezo kwa utafiti wake huo kwa wanahabari, watafiti wa usoni, wanajamii na wengineo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:50
Last Modified: 13 Jul 2016 10:50
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1194

Actions (login required)

View Item View Item