Usawiri wa Ujinsia Katika Filamu: Uchunguzi wa Matumzi ya Lugha Katika Filamu za Steven Kanumba

Suwed, Ahmad Abdalla (2013) Usawiri wa Ujinsia Katika Filamu: Uchunguzi wa Matumzi ya Lugha Katika Filamu za Steven Kanumba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of SUWED-TASNIFU_FINAL-Version.pdf]
Preview
PDF
Download (785kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu usawiri wa ujinsia katika filamu uchunguzi wa matumizi ya lugha katika filamu za Steven Kanumba. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza usawiri wa kijinsia katika lugha ya filamu za Steven Kanumba ili kuona ni jinsi gani lugha inatumika kusawiri masuala ya kijinsia katika jamii. Utafiti huu ulitumia mbinu nne za ukusanyaji data ambazo ni; maktaba, usaili, dodoso na majadiliano ya vikundi. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya; madhumuni maalum na utuezi nasibu wa sampuli. Utafiti huu umegundua kuwa, filamu za Kanumba zimetumia lugha kwa namna ambayo inasawiri mahusiano ya kijinsia katika jamii mbalimbali hususani jamii ya Watanzania na Afrika. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa Kanumba katika filamu zake ametumia zaidi kejeli na dhihaka kuliko vipengele vingine vya lugha. Matumizi ya kejeli na dhihaka yanaonyesha ndiyo mbinu ya kifani inayotawala kazi za Kanumba. Utafiti huu umedhihirisha kuwepo kwa usawiri wa mwanamke kwa namna mbalimbali. Katika kazi za fasihi za Kanumba imedhihirika kwamba mwanamke anasawiriwa kama mama, chombo cha starehe, kiumbe dhaifu na tegemezi, kiumbe kisichokuwa na maamuzi binafsi, chanzo cha matatizo, msaliti, na ni kiumbe mvumilivu na mnyenyekevu. Utafiti huu pia umebaini kuwa, matumizi ya lugha katika filamu za Steven Kanumba yanadhihirisha tofauti baina ya mwanamke na mwanaume katika jamii. Imegundulika kuwa kuna mahusiano tofauti baina ya mwanamke na mwanaume. Tofauti ya mahusiano haya imejengeka katika misingi ya kijamii ambapo tangu awali jamii inawaona wanaume ni tofauti na wanawake.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 27 Apr 2016 09:41
Last Modified: 27 Apr 2016 09:41
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1079

Actions (login required)

View Item View Item