Yoradi, Sikombe Yizukanji
(2013)
Lugha ya Kiswahili katika Kufundishia na Kujifunzia Elimu Shule za Sekondari.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Azma ya utafiti huu, ilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kufundishia na kujifunzia Elimu shuleni na Vyuoni. Utafiti huu umefanywa Wilayani Mvomero.Taasisi tatu zilishirikishwa. Shule za Msingi, Shule za Sekondari, Vyuo vya elimu. Masomo mawili Kiswahili na Kiingereza yalichunguzwa. Njia zilizotumika katika utafiti huu zilikuwa ni utafiti wa Maktabani, ana kwa ana na Masikanini .Matokeo ya Utafiti huu yamebaini kwamba; Kiswahili ni Lugha inayoeleweka vizuri zaidi katika kufundishia na kujifunzia elimu shuleni kuliko lugha ya kiingereza. Watoto wengi hawaelewi lugha ya Kiingereza pale inapotumiwa kama lugha ya kufundishia na kuwafanya watoto wasiweze kupata elimu ambayo wangeipata shuleni kwa ajili ya kuliendeleza Taifa.
Actions (login required)
|
View Item |