Muro, Upendo
(2025)
Kuchunguza Saikolojia ya Mhusika na Mbinu za Kisanaa katika Riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Saikolojia ya mhusika katika riwaya ya Kiswahili ni mada inayovutia katika macho ya msomaji na masikio ya msikilizaji hasa anapobaini kuwa riwaya iliyotafitiwa ni Wasifu wa Siti Binti Saad. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza saikolojia ya mhusika katika riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad. Lengo hili lilivunjwa katika malengo mahususi mawili ambayo yalikuwa ni kubainisha mambo yanaoibua saikolojia ya mhusika Siti katika riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad na kuchambua mbinu za kisanaa zilizotumika kuibua saikolojia ya mhusika Siti katika riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka maktabani. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa katika riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad saikolojia ya mhusika Siti inajitokeza katika masuala ya maisha ya dhiki kijijini, changamoto ya elimu, kupambana na mila na desturi, moyo wa kujaribu, ubunifu wa Siti na kutokukata tamaa katika maisha. Ndani ya mambo haya matano kunajitokeza saikolojia ya mhusika wa Siti. Kwa upande wa mbinu za kisanaa matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa kuna matumizi ya tashibiha, sitiari, nyimbo na mtindo. Katika utafiti huu tumetumia nadharia ya Saikolojia Changanuzi kuchambua data za utafiti na kushadadia hoja zilizotokana na matokeo ya utafiti. Mapendekezo Utafiti zaidi kuhusu saikolojia ya mhusika au wahusika unaweza kufanywa katika riwaya za watunzi mbalimbali ili kutoa picha kamili ya saikolojia ya wahusika katika riwaya ya Kiswahili. Pia wahusika wengine katika riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad walivyochangia katika kujenga saikolojia ya mhusika Siti ambaye ni mhusika mkuu katika riwaya hiyo.
Actions (login required)
 |
View Item |