Ulinganishi wa ujumbe wa methali za Kiswahili katika Jamii ya Wazanzibar aya za Qur-an.

Khamis, Ali Juma (2025) Ulinganishi wa ujumbe wa methali za Kiswahili katika Jamii ya Wazanzibar aya za Qur-an. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA ALI JUMA KHAMISI FOR BLACK BOOK.docx] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (133kB)
Official URL: http://www.out.ac.tz

Abstract

Utafiti huu unahusu Ulinganishi wa Ujumbe wa Methali za Kiswahili katika Jamii ya Wazanzibar na Mafunzo ya Aya za Qur-an. Utafiti huu unakusudia kuchunguza kwa kina uhusiano uliopo kati ya methali za Kiswahili zinazotumika katika jamii ya Wazanzibar na mafunzo ya Qur-an, kwa kutumia nadharia ya Sosholojia. Nadharia hii inachukulia kazi ya fasihi kama kioo cha jamii kinachoakisi maisha, mitazamo, na mienendo ya wanajamii. Kwa msingi huo, utafiti huu unachunguza namna methali za Kiswahili zinavyobeba mitazamo, maadili, na falsafa za kijamii zinazolingana na mafundisho ya Qur-an. Kwa mujibu wa nadharia ya Sosholojia, fasihi haiwezi kutenganishwa na mazingira ya kijamii na kihistoria yaliyoizalisha. Hivyo basi, utafiti huu unazingatia kuwa methali za Wazanzibar ni zao la jamii yenye misingi ya Kiislamu na maadili ya Kiswahili, ambapo dini na utamaduni vimeungana katika kujenga mfumo wa maadili unaoelekeza mwenendo wa jamii. Kwa hivyo, methali na aya za Qur-an zote zinaweza kuchunguzwa kama vielelezo vya fikra na mitazamo ya kijamii kuhusu maadili, haki, usawa, na uhusiano wa binadamu. Aidha, methali za Kiswahili zinavyowasilisha ujumbe wa kijamii unaolingana na mafundisho ya Qur-an katika kujenga uadilifu, haki, heshima, utiifu, umoja na mshikamano, uvumilivu na subira, uadilifu katika uchumi na utawala na maadili ya kifamilia na kijamii. Kwa msingi wa Usosholojia, ujumbe wa methali za Kiswahili na mafunzo ya aya za Qur-an ulichambuliwa kwa kuzingatia uhusiano uliopo katika muktadha wa jamii ya Wazanzibar, jamii yenye historia ya uislamu, biashara, elimu nakadhalika. Kupitia mlinganisho huu, utafiti umedhihirisha kuwa methali hazijajitokeza tu kama maneno ya hekima, bali kama zana za kijamii zinazoweka kanuni za maadili na mwenendo wa maisha unaoendana na mafundisho ya dini ya Kiislamu.Vilevile, utafiti huu utatoa mchango katika taaluma ya fasihi na elimu ya Kiislamu kwa kuonesha kwamba kati ya dini na utamaduni kuna mwingiliano wa kijamii unaoweza kueleweka kupitia misemo ya hekima.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Jan 2026 14:19
Last Modified: 30 Jan 2026 14:19
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/5004

Actions (login required)

View Item View Item