Taswira za ushujaa na uzalendo zinavyoibuwa hali halisi ya kisiasa katika maisha: Tamthilia teule za Emmanuel Mbogo.

Muhidin, Faida Fakih (2025) Taswira za ushujaa na uzalendo zinavyoibuwa hali halisi ya kisiasa katika maisha: Tamthilia teule za Emmanuel Mbogo. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA FAIDA MPYA KABISA.docx] PDF - Submitted Version
Available under License Creative Commons Attribution.

Download (127kB)
Official URL: http://www.out.ac.tz

Abstract

Utafiti huu umelenga kuchunguza taswira za ushujaa na uzalendo zinavyoibua hali halisi ya kisiasa katika maisha kupitia tamthilia za Emmanuel Mbogo za Nyerere na Safari ya Kanaani na Mondlane na Samora. Utafiti umeongozwa na malengo mahasusi matatu ambayo ni; kubainisha taswira zilizotumika katika tamthilia teule za Mbogo; kuchambua aina za taswira zinazowasilisha dhamira za uzalendo na ushujaa katika tamthilia teule za Mbogo pamoja na kuchambua jinsi taswira za ushujaa na uzalendo zinavyosawiri hali halisi ya kisiasa katika tamthilia za Mbogo. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Simiotiki. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa zipo taswira mbalimbali katika tamthilia hizi zinazohusiana na uzalendo na ushujaa. Katika lengo la kwanza, utafiti umeonesha taswira kama vile, taswira za utungu na maumivu ya Wanaafrika ambazo zilionesha matatizo yaliyowakumba Wanamsumbiji katika kupigania uhuru kutoka katika tamthilia ya Mondlane na Samora na taswira za misimamo ya mwalimu Nyerere katika kusimamia siasa za ujamaa katika tamthilia ya Nyerere na Safari ya kanaani. Lengo la pili limebainisha aina mbalimbali za taswira na namna zilivyoweza kutoa sura ya maisha na mapitio ya nchi za Kiafrika kabla na mara tu baada ya uhuru wanchi hizo kama ilivyooneshwa kwa nchi za Msumbiji (kabla ya uhuru) na Tanzania (baada ya uhuru). Lengo la tatu limechambua na kuonesha jinsi taswira zilizochambuliwa katika malengo mawili yaliyotangulia zilivyosawiri hali halisi ya kisiasa. Maneno Makuu: Taswira, Simiotiki, Uzalendo

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Jan 2026 14:10
Last Modified: 30 Jan 2026 14:10
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/5003

Actions (login required)

View Item View Item