Labiswai, Marko L.
(2025)
Athari za Makosa yatokanayo na Fonolojia ya Kigogo katika Semantiki ya Kiswahili Sanifu: Mifano kutoka kwa Wazungumzaji wa Kigogo.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulichunguza Athari za Makosa yatokanayo na Fonolojia ya Kigogo katika Semantiki ya Kiswahili Sanifu: Mifano kutoka kwa Wazungumzaji wa Kigogo. Utafiti ulifanyika katika shule mbili za kata ya Matongoro wilayani Kongwa. Data za utafiti zilikusanywa kwa mbinu ya ushuhudiaji shirikishi na dodoso. Sampuli ya utafiti iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Data za utafiti zilichanganuliwa kwa mkabala wa kimaelezo kwa kuongozwa na nadharia ya uchanganuzi makosa iliyoasisiwa na Corder 1967. Matokeo ya utafiti huu yalibaini makosa mbalimbali ya kifonolojia. Makosa hayo ni pamoja na; ubadilishaji wa sauti, udondoshaji wa sauti na uchopekaji wa sauti. Athari za makosa hayo katika maana za maneno ya Kiswahili sanifu zilikuwa ni pamoja na; upotoshaji wa maana, kubadili maana na kukwamisha mawasiliano. Mbinu zilizopendekezwa kutumika ili kuepuka makosa hayo zilikuwa ni; Kuwahamasisha wanafunzi kuzungumza lugha ya Kiswahili muda wote wakiwa katika mazingira ya shule, somo la Kiswahili kufundishwa na walimu mahiri wa lugha ya Kiswahili, wazazi na walezi kuhamasishwa kuzungumza na watoto wao lugha ya Kiswahili katika mazingira ya nyumbani, wanafunzi wapewe nafasi na muda wa kutosha kuzungumza lugha ya Kiswahili shuleni na wanafunzi wanaojitahidi kufanya vizuri katika kuzungumza Kiswahili wapewe zawadi ili iwe motisha kwa wenzao.
Actions (login required)
 |
View Item |