Haji, Maimuna
(2022)
Kuchunguza Matumizi ya Semi zilizoandikwa katika Kuta za Nyumba za Vijiji: Mfano Kutoka Pemba.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni “Kubainisha na kuchambua dhamira na vipengele vya lugha katika semi zinazoandikwakwenye nyumba za vijiji za Pemba.” Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi matatu ambapo lengo mahususi la kwanza lilikuwa ni; “Kuzianisha semi zinazopatikana katika kuta za nyumba za vijiji kisiwani Pemba.” Lengo hili liliongozwa na swali la utafiti lisemalo; “Ni semi zipi zinazopatikana katika kuta za nyumba za vijiji za Pemba?” Lengo mahususi la pili lilikuwa ni “Kubainisha matumizi ya lugha katika semi zinazopatikana katika kuta za nyumba za vijiji za Pemba.” Lengo hili liliongozwa na swali la utafiti lisemalo “Ni vipengle vipi vya lugha vinavyopatikana katika semi zinazopatikana katika kuta za nyumba za vijiji za Pemba?” Na lengo mahususi la tatu lilikuwa ni “Kutathmini dhamira zinazojitokeza katika semi zinazopatikana katika kuta za vijiji za Pemba.” Lengo hili liliongozwa na swali la utafiti lisemalo “Ni dhamira zipi zinazopatikana katika semi zinazoandikwa katika kuta za nyumba za vijiji za Pemba?” Data za utafiti huu zilikusanywakwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji na kuchambuliwa kwa mkabala wa kimaelezo sambamba na nadharia za Simiotiki na Mwitiko wa Msomaji. Matokeo ya utafiti huu yameonesha semi ziandikwazo kwenye kuta za nyumba za vijiji za Pemba zinaweza kuwekwa katika makundi ya semi zenye kuonesha utabaka, kuhimiza mshikamano, kuonesha imani, kuhamasisha kazi, kukosoa, kukejeli, kuonesha utamaduni, mapenzi na kuifunza jamii.Kwa upande wa lugha inayotumika katika semi ziandikwazo katika kuta za nyumba za vijiji za Pemba utafiti umebainikuwa semi hizo zinatumia lugha ya lahaja, balagha, kejeli, tashihisi, misemo, methali na takiriri. Aidha, dhamira zinazopatikana katika semi hizo ni kuburudisha, kuifunza jamii, kukosoa, mapenzi, kukejeli, itikadi, uchumi, wivu na usimamizi wa haki.
Maneno Makuu:Kuta, Vijiji, Itikadi
Actions (login required)
|
View Item |