Kuchunguza Dhamira za Kijamii katika Mashairi ya Tigiti Sengo: Mfano Kutoka katika Diwani ya Midulu.

Abdulrahaman, Mohamed Salim Khaiar (2020) Kuchunguza Dhamira za Kijamii katika Mashairi ya Tigiti Sengo: Mfano Kutoka katika Diwani ya Midulu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA MOHAMED SALIM KHAIAR ABDULRAHAMAN MPYA 1.docx] PDF - Submitted Version
Download (114kB)

Abstract

Mada ya utafiti huu ilikuwa inahusu‘Kuchunguza Dhamira za Kijamii katika Mashairi ya Tigiti Sengo: Mfano Kutoka katika Diwani ya Midulu’ Diwani ya Midulu. Ili kutimiza kusudi hilo tulikuwa na malengo mahsusi mawili. . Kubainisha dhamira za kijamii katika Diwani ya Midulu na la pili lilikuwa ni kufafanua uhalisia wa dhamira za kijamii Diwani ya Midulu. Data za msingi zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa mkabala wa kimaelezo. Mjadala wa data uliongozwa na nadharia za Usosholojia. Matokeo yanaonesha kuwa Diwani ya Midulu ina utajiri mkubwa uliomo katika dhamira. Diwani ya Midulu Dhamira hizo ni umasikini, masuala ya ndoa, kuheshimiana, ushirikiano, kujitegemea, malezi na dhuluma. Dhamira hizi zina uhalisia katika maisha ya kila siku ya jamii kwa kuwa zinagusa maisha ya Watanzania wengi. Utafiti huu unapendekeza kuundwa kwa mikakati imara inayolenga kuendeleza misingi ya uandishi wa ushairi wa Kiswahili, pamoja na kulinda kazi za waandishi kisera na kisheria. Aidha, wasanii wajenge utashi utakaotawala vema kazi zao ili waweze kumudu ushindani wa kazi za kisanaa, kimaudhui na kiwakati. Maneno Makuu: Dhamira, Midulu, Mkabala, Diwani.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 08 Apr 2022 06:10
Last Modified: 08 Apr 2022 06:10
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3135

Actions (login required)

View Item View Item