Jeremiah,, Lucas
(2019)
Uchanganuzi wa
Kishazi Tegemezi cha Kisukuma: Mtazamo wa X-Baa”,.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Uchanganuzi wa Kishazi Tegemezi Cha Kisukuma kwa mtazamo wa x-baa ni mada
ambayo utafiti wake iliyofanyika kwa kushirikisha watafitiwa 98. Utafiti huu
ulifanyika katika Wilaya ya Geita vijijini Mkoa wa Geita. Utafiti huu ulifanyika kwa
lengo uchanganuzi wa kishazi tegemezi cha kisukuma kinavyojitokeza katika lugha
hiyo.Katika kukamilisha adhima hiyo tulikusanya data kwa kutumia mbinu za
makitabani,hojaji na mahojiano. Mbinu zilizotumika kupata watafitiwa wa utafiti huu
ni mbinu ya makusudi kutoka kwa watafitiwa 98 walioshiriki katika utafiti huu
ambao wametoka shule ya Bukondo, chigunga, Nyachiluluma. Butundwe, Nyamigota,
kaseme` Katoro na Lutozo Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ile ya X-Baa
ndiyo iliyotumika katika kuchanganulia vishazi tegemezi vya kisukuma.Nadharia hii
husaidia kuchanganua kirai, kishazi na sentensi kwa kutekeleza majukumu haya;
kubainisha miundo ya virai kwa uwazi, kueleza mahusiano ya vipashio katika kirai
nomino, kuonyesha jinsi umilikaji unavyojitokeza baina ya vipashio na vingine na
mwisho kuonyesha kanuni za kijumla katika kufafanua muundo wa vishazi. Kwa hiyo
utafiti ufanyike zaidi katika uchanganuzi wa vishazi vya lugha nyingine za kibantu na
tungo ambazo utafiti huu haukufanyika katika lugha hii ya kisukuma kwa kutumia
nadharia ya x-baa.
Actions (login required)
|
View Item |