Felician, Frederick
(2019)
Makosa ya Kifonolojia Yanayofanywa na Wazungumzaji wa Kihaya Wanaojifunza
Kiswahili Sanifu.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu umechunguza wa makosa ya kifonolojia yanayofanywa na wazungumzaji
wa Kihaya wanaojifunza Kiswahili sanifu. Malengo ya Utafiti huu yalikuwa ni (a)
Kubainisha makosa ya kifonolojia yanayofanywa na wazungumzaji wa Kihaya katika
ujifunzaji wa Kiswahili sanifu (b) Kubainisha sababu za wazungumzaji wa Kihaya
kufanya makosa ya kifonolojia katika kujifunza Kiswahili sanifu (c) Kubainisha
mbinu za kutumia ili kuwasaidia wazungumzaji wa Kihaya wanaojifunza Kiswahili
sanifu kama L2 kwao. Njia zilizotumika kukusanya data ni hojaji ilitumika kwa
watafitiwa ambao ni wanafunzi, walimu na wazazi, mahojiano ambayo ilitumika kwa
walimu na wazazi wazungumzaji wa Kihaya na Kiswahili na usomaji makini ambayo
ilitumika kupitia kwa umakini kazi mbalimbali za wanafunzi ili kubaini makosa ya
kifonolojia. Data ya utafiti huu imechanganuliwa kwa makabala wa kimaelezo kwa
kuongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makosa ya Corder (1967). Matokeo ya utafiti
yanaonesha makosa yanayofanywa kuwa ni pamoja na matumizi ya sauti mbadala
kwa sauti ambazo hazipo katika mfumo wa lugha ya Kihaya ila zipo katika Kiswahili
sanifu, kuchanganya sauti, udondoshaji na uchopekaji wa sauti. Sababu za
wazungumzaji wa Kihaya kufanya makosa ya kifonolojia katika kujifunza Kiswahili
sanifu zipo kama ifuatavyo; utofauti wa mifumo ya sauti kati ya lugha hizi mbili,
ufundishaji mbaya wa lugha ya pili, walimu kutokuwa na taaluma ya fonetiki
matamshi na matumizi ya Kihaya muda mwingi kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa
ujumla. Mbinu za kuwasaidia wanafunzi hawa ni pamoja na wazazi, wanafunzi na
jamii nzima ya wazungumzaji wa lugha ya Kihaya kutambua umuhimu wa Kiswahili,
taaluma ya fonetiki matamshi kutolewa ngazi zote za elimu, matumizi ya mbinu bora
za ufundishaji wa lugha ya pili.
Actions (login required)
|
View Item |