Athari za Lugha ya Kinyaturu katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili

Mangi, Joyce Elia (2019) Athari za Lugha ya Kinyaturu katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU - JOYCE MANGI.pdf] PDF
Download (872kB)

Abstract

Utafiti huu uulilenga kuchunguza athari ya lugha ya Kinyaturu katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili ili kubainisha changamoto na mwisho kutoa mapendekezo ya suluhisho la changamoto hizo. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu; Kwanza, kubainisha athari za lugha ya Kinyaturu katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wanaozungumza Kinyaturu kama lugha yao ya kwanza. Pili, kubainisha sababu za athari hizo kwa wazungumzaji wa Kinyaturu wanaojifunza lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili. Tatu, kupendekeza mbinu mbalimbali zitakazotumika kuwasaidia wanafunzi walioathiriwa na Kinyaturu wanapojifunza lugha ya Kiswahili. Aidha, utafiti huu ulifanyika katika eneo la Singida Vijijini ambapo data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu kuu tatu; usomaji wa maandiko, mahojiano na hojaji. Wahojiwa waliteuliwa kwa njia ya usampulishaji makusudi na nasibu. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano (NKM). Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, athari za lugha ya kinyaturu katika ujifunzaji wa kiswahili ziko kwenye kisemantiki (kimaana), kimsamiati, na kimatamshi. Mtafiti aliweza kubaini mbinu ambazo zinaweza kutumika katika kuwasidia wanafunzi walioathilika kwa lugha ya awali wanapojifunza lugha ya kiswahili. Mbinu hizo ni, watoto wafundishwe lugha ya Kiswahili tangia utotoni, walimu wanapaswa kuwa mahiri katika kufundisha lugha ya kiswahili, kuwe na mazingira rafiki ya kujifunza lugha ya kiswahili, wazazi au walezi wa watoto wahamasishwe kutumia lugha ya kiswahili. Kwa mujibu wa utafiti huu zipo sababu zinazosababisha kutokea kwa athari za lugha ya kinyaturu katika kujifunza lugha ya kiswahili kama ufundishaji mbaya wa somo la kiswahili, lugha ya kiswahili kutopewa kipaumbele, kudumisha utamaduni wa kinyaturu, mazingira duni ya kujifunza lugha ya kiswahili, lugha ya kinyaturu hutumika kama utambulisho

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 23 Sep 2021 09:16
Last Modified: 23 Sep 2021 09:16
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3011

Actions (login required)

View Item View Item